Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 7 7

M U N G U B A B A

mahali yanakusifu, na utukufu wako umefunuliwa katika Yesu Kristo Mwokozi wetu. Kwa hivyo tunakusifu, utatu mtukufu na mtakatifu, Mungu mmoja, milele na milele. Amina. ~ Kanisa la Kipresbiteri la Marekani na Kanisa la Kipresbiteri la Cumberland, Kitengo cha Theolojia na Huduma ya Kuabudu. Kitabu cha Ibada ya Pamoja. Louisville, KY.: Westminister/John Knox Press, 1993. uk. 51 Ee Baba, tumaini langu, Ee Mwana, kimbilio langu, Ee Roho Mtakatifu, ulinzi wangu. Utatu mtakatifu, utukufu ni wako. ~ Compline, Eastern Orthodox, St. Joannikios

Appleton, George, mhariri. The Oxford Book of Prayer. Oxford/New York: Oxford University Press, 1988. uk. 183

Weka kando vitabu na madokezo yako, kusanya mawazo na tafakari zako, na ufanye jaribio la Somo la 2, Mungu kama Muumba: Utawala wa Mungu.

Jaribio

3

Mazoezi ya kukariri maandiko

Fanya mazoezi pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu kwa kutamka andiko la kukumbuka ulilopewa katika kipindi kilichopita: 1 Mambo ya Nyakati 29:11-12.

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walikusudia kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za kukusanya

MIFANO YA REJEA

Imani Isiyoleta Maana?

Mmoja wa washirika wa kanisa lako, Bi. Jackson, alitembelewa na Shahidi wa Yehova juzijuzi, na tangu wakati huo mazungumzo hayo yanamsumbua. Kwa zaidi ya saa moja Bi. Jackson alisikiliza kwa makani mantiki safi, sahihi, na yenye kuvutia ya Mashahidi waliomtembelea nyumbani kwake. Alihisi kulemewa kabisa wageni hawa walipokuwa wakielezea orodha ya makosa ambayo walisema makanisa mengi huamini. Wakiyakataa makosa mengi na kusema kwamba ni uongo na uvumi tu wa kihistoria, Mashahidi hawa walitoa hoja kwa dhati kabisa dhidi ya fundisho kwamba Roho Mtakatifu ni nafsi, fundisho la Utatu, uungu wa Kristo, uwepo wa kuzimu, wokovu kwa neema, na mengine mengi. Akiwa amechanganyikiwa,

1

page 290  3

Made with FlippingBook - Share PDF online