Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
/ 7 9
M U N G U B A B A
Mungu katika Utatu: Ukuu wa Mungu Sehemu ya 1: Ukuu wa Mungu (Sifa za Asili)
YALIYOMO
Mch. Dkt. Don L. Davis
Neno la Mungu kwa uwazi linasisitiza kwamba kuna Mungu mmoja tu ( Shema, Kum. 6:4), na bado pia linathibitisha uungu wa Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Fundisho la Utatu ni matokeo ya kukubali fundisho la Biblia juu ya umoja wa Mungu, na wakati huohuo, likithibitisha yale linayosema kuhusu asili ya uungu ya nafsi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Lengo letu katika Sehemu hii, Ukuu wa Mungu, ni kukuwezesha kuona kwamba: • Fundisho la Utatu hurejelea fundisho la Biblia kuhusu utatu wa nafsi ya Mungu. • Maandiko yanasema kwamba Mungu ni mmoja, na kwamba hakuna mwingine ila yeye aliye Mungu mmoja, na bado yanasisitiza kwamba Mungu huyo mmoja hujidhihirisha mwenyewe kama Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. • Kila mshiriki wa Utatu (Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu) anazo sifa na hufanya kazi ya Mungu, anaitwa Mungu, na hutumia mamlaka kama Mungu. • Biblia inathibitisha umoja na wingi wa Mungu kadhalika (kwamba Uungu Mtakatifu ni zaidi ya nafsi moja), kwa pamoja nafsi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu zinazungumzwa kama nafsi katika Uungu Mtakatifu. • Kanisa limejaribu kutengeneza namna za kuelewa mafunidisho ya Biblia kuhusu Utatu, huku pakiwa na viwango tofauti vya kukubalika kwayo miongoni mwa waamini. • Ni lazima tusisitize asili ya Mungu ya utatu, tukithibitisha kwamba washiriki wa Utatu, ingawa ni Mungu katika nafsi tatu, kimsingi ni umoja, wana utofauti, na usawa, kwa pamoja wakimkamilisha Mungu mmoja wa kweli, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.
Muhtasari wa Sehemu ya 1
3
Made with FlippingBook - Share PDF online