Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

1 0 /

M U N G U M W A N A

Matokeo ya mwisho wa kozi yatatolewa katika mfumo wa gredi kwa kutumia skeli ya kutunuku matokeo kwa mtindo wa herufi zenye alama chanya na hasi, kisha alama za gedi yako ya ufaulu katika kazi mbali mbali zitajumlishwa na kugawanywa kwa idadi ya kazi na vipimo vingine husika ili kupata wastani wa matokeo yako ya mwisho. Kuchelewesha au kushindwa kabisa kukabidhi kazi zako kutaweza kuathiri matokeo yako. Hivyo, ni vyema kupangilia shughuli na muda wako mapema na kuwasiliana na mkufunzi wako endapo kutakuwa na changamoto yoyote. Kama sehemu ya ushiriki wako katika moduli hii ya Mungu Mwana ya mataala wa Capstone , utahitajika kufanya kazi ya ufafanuzi (uchunguzi wa ndani ya Maandiko yenyewe) wa mojawapo ya vifungu vifuatavyo vya Maandiko:  Yohana 1:14-18  Tito 2:11-14  Waebrania 1:5-14  Waebrania 2:14-17  Wakolosai 1:13-20  1 Timotheo 3:16  Wafilipi 2:5-11 Kusudi la kazi hii ya ufafanuzi (eksejesia) ni kukupa fursa ya kufanya uchunguzi wa kina wa kifungu muhimu kimojawapo kinachozungumza juu ya asili na kazi ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Uongozi wa Kikristo kimsingi umejengwa juu ya kweli kuhusu Yesu. Haiwezekani wala haiaminiki kwamba mtu anaweza kuwa mhudumu mzuri wa Injili huku akiwa na ufahamu potofu, wa chini na wa aibu kuhusu Yesu. Kwa maana moja, makosa katika fundisho hili ni hatari sio tu katika eneo la imani, lakini pia yanalemaza katika eneo la ufuasi, huduma, na utumishi. Katika Wakolosai, Paulo anasisitiza kwamba Yesu Kristo pekee ndiye kiini cha huduma yoyote; “...ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo” (Kol. 1:28). Kuinuka na kuanguka kwa huduma ya Kikristo kunategemeana na kuwepo au kutokuwepo kwa mwitikio sahihi, wa kibiblia, na wenye kicho cha maisha kwa Maandiko kuhusiana na uungu na ubinadamu wa Yesu, Mwana wa Mungu. Kwa hiyo, kazi hii itakupa fursa ya kutumia mojawapo ya maandiko hapo juu kama msingi wa kuchunguza ufahamu wako juu ya uhusiano wa andiko husika na Yesu Kristo. Unaposoma moja ya maandiko hapo juu (au maandiko ambayo wewe na Mkufunzi wako mtakubaliana ambayo yanaweza kuwa hayapo kwenye orodha hii), tunatumai kuwa uchambuzi wako wa maandiko hayo utakuwekea wazi zaidi asili ya utukufu wa mtu huyu ambaye tumejitolea maisha yetu yote kumtumikia na Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko (Eksejesia)

Dhumuni

Made with FlippingBook - Share PDF online