Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
1 0 6 /
M U N G U M W A N A
C. Tunaweza kupata kweli gani kutokana na mtazamo huu?
1. Kifo cha Yesu ni udhihirisho wa ajabu wa upendo wa Mungu kwetu (Yoh. 3:16).
2. Kifo cha Yesu, wakati huo huo, ni onyesho la ghadhabu ya Mungu dhidi ya dhambi (1 Yoh. 2:2).
3. Upendo wa Mungu uliodhihirishwa msalabani unapaswa kutusukuma kumtafuta, na si kutufanya tufikiri tunaweza kuepuka hukumu ikiwa tutapuuza dhabihu yake (Rum. 2:3-5).
III. Mtazamo wa Tatu: Kifo cha Yesu kama udhihirisho wa haki ya kiungu ( nadharia ya kiserikali )
Bwana wetu alipofufuka katika
3
wafu, na kuyakanyaga mauti chini ya miguu yake, na kumfunga mwenye nguvu, na kumweka huru mwanadamu, ndipo uumbaji wote ukaona wazi kwamba kwa ajili ya mwanadamu Hakimu alihukumiwa. ~ Melito (c. 170), 8.756. Ibid. uk. 42.
A. Waandishi na hoja za wale walio na mtazamo wa kiserikali :
1. Watetezi wa mtazamo huu: Hugo Grotius, mwanasheria (1583-1645)
2. Mungu mwenye haki ameweka sheria, na dhambi inakiuka sheria hizo.
3. Ingawa Mungu ana haki ya kuadhibu dhambi, si lazima afanye hivyo.
4. Mungu anatenda kazi ili kudumisha “maslahi ya serikali,” halazimiki kuadhibu kila uasi mahususi wa sheria zake.
a. Anatenda kwa ajili ya maslahi bora ya wanadamu.
Made with FlippingBook - Share PDF online