Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
1 0 8 /
M U N G U M W A N A
3. Maoni yasiyo ya kibiblia ambayo hayatoi ufahamu wa kimaandiko kamwe hayawezi kuelezea kwa usahihi maana ya kifo cha Yesu (Isa. 8:20).
IV. Mtazamo wa Nne: Kifo cha Yesu kama ushindi dhidi ya nguvu za dhambi na uovu ( Nadharia ya Fidia )
Katika nyakati za mwisho, Mwana alifanywa kuwa mwanadamu kati ya wanadamu, na Alitengeneza upya jamii ya wanadamu. Hata hivyo, Alimwangamiza na kumshinda adui wa mwanadamu. Basi akaipatia kazi ya mikono yake ushindi dhidi ya adui. ~ Irenaeus (c. 180, E/W), 1.495. Ibid. uk. 43.
A. Waandishi na hoja za wale wanaoshikilia mtazamo wa Fidia :
1. Watetezi wa mtazamo huu:
a. Baba wa Kanisa la Kwanza, Origen; (mtazamo wake ulitawala mtazamo wa awali wa Kanisa; kwa sababu ya imani hii ya awali, mtazamo huu unaitwa “mtazamo wa kitambo”)
3
b. Gustaf Aulen: Christus Victor : Utafiti wa Kihistoria wa Aina Tatu Kuu za Dhana ya Upatanisho.
2. Ulimwengu mzima umenaswa katika tamthilia ya ulimwengu: nguvu za wema zinafanya vita dhidi ya nguvu za uovu.
3. Katika vita hivi, Shetani alipata udhibiti wa ulimwengu na wakaazi wake.
4. Ibilisi sasa ana haki za kisheria juu ya mwanadamu; fidia lazima ilipwe kwa shetani ili kuwakomboa wakazi wake.
a. Nukuu za Biblia: (1) Mathayo 20:28 (2) Marko 10:45
Made with FlippingBook - Share PDF online