Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

1 1 0 /

M U N G U M W A N A

C. Tunaweza kupata kweli gani kutokana na mtazamo huu?

1. Kifo cha Yesu ndicho kilele cha vita vya Mungu dhidi ya uovu, kifo, na nguvu za laana (1 Yoh. 3:8).

2. Kifo cha Yesu kinawakilisha uharibifu kamili wa uwezo wa Ibilisi wa kutushtaki, kututawala kupitia nguvu za kifo, na kutulaumu kama wenye dhambi tusiostahili mbele za Mungu (1 Pet. 5:8-10).

3. Tunashinda nguvu za uovu kupitia yale ambayo Yesu alitimiza msalabani; Ibilisi hakuwa na haki ya kulazimisha chochote juu yetu (2 Kor. 2:14).

V. Mtazamo wa Tano: Kifo cha Yesu kama kumpa Mungu malipo stahiki ( Nadharia ya Kuridhika )

Kwa mateso yake mwenyewe, alituokoa kutoka katika makosa na dhambi. ~ Klementi wa Aleksandria (c. 195, E), 2.257. Ibid. uk. 44.

3

A. Waandishi na hoja za wale wanaoshikilia mtazamo wa Kuridhika :

1. Watetezi wa mtazamo huu: Baba wa Kanisa la Kwanza, Anselm. Cur Deus Homo? ( Kwanini Mungu Mwanadamu? )

a. Alitaka kutoa jibu la kwa nini Mungu alifanyika mwanadamu.

b. Mtazamo huu unasisitiza kwamba kitu fulani katika asili ya Mungu kilidai (si kama malipo kwa Ibilisi, yaani, maoni ya Fidia).

2. Dhambi ni kutompa Mungu kile anachostahili; ni kumvunjia Mungu heshima kwa kutompa heshima na utukufu anaostahili.

Made with FlippingBook - Share PDF online