Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 1 1 7

M U N G U M W A N A

yaliyopo hapa chini yametolewa ili kuibua maswali yako mwenyewe kuhusu kifo cha Yesu, yanayoendana zaidi na muktadha wako. * Je, kitendo cha Yesu Kristo kujifanya kuwa hana utukufu kinapaswa kuathiri vipi mitazamo yetu kuhusu maisha na huduma zetu tunapoitikia wito wa Mungu maishani mwetu? * Unyenyekevu na kujishusha kwa Yesu ni kielelezo kwetu kwa kadiri gani, na kujitiisha kwake kwa Baba ni tendo linalompasa yeye peke yake ? Elezea jibu lako. * Je, kwa sasa unatumiaje maagizo ya Yesu yafuatayo katika maisha na huduma yako? Luka 9:23-25 ​– “Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. 24 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. 25 Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?” * Ni kwa njia gani tunapaswa kujumuisha maandiko kama Wafilipi 2:5-11 na 2 Wakorintho 8:9 katika ufahamu wetu wa ufuasi wa Kikristo na huduma? * Kati ya picha zote zinazotolewa kuhusu kifo cha Yesu na maana yake katika maisha yetu, ni ipi ambayo wewe binafsi unaiona kuwa yenye nguvu zaidi kwa habari ya maisha na huduma yako? * Malizia sentensi ifuatayo: “Jambo moja ambalo bado linanitatiza kuhusu jinsi ninavyoelewa kifo cha Yesu ambalo nahitaji kujifunza zaidi ni _____ ______________________________.” * Ni njia zipi ambazo utatafuta kufanya kifo cha Yesu kuwa halisi zaidi katika maisha na huduma yako? Kwa nini Meza ya Bwana ni tendo muhimu sana linaloendelea kutusaidia kufahamu maana ya mateso na kifo chake kwa niaba yetu? * Tunawezaje kufundisha vizuri zaidi unyenyekevu na kifo cha Yesu katika kuwafuasa wanafunzi wetu, kuhubiri, na kufundisha? Jadilini kwa pamoja njia mnazoweza kusisitiza tena mateso ya Kristo katika maisha ya makanisa yenu.

3

Made with FlippingBook - Share PDF online