Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 1 2 7

M U N G U M W A N A

na habari njema za Kristo. Ni maono ya kuwezesha, kubadilisha, na kutia hamasa, na ambayo yanahitaji kugunduliwa na kuamshwa tena katika siku na nyakati zetu. Tunachohitaji sisi katika huduma ya mijini leo ni hisia na mawazo yetu kutekwa tena na maono hayo yanayotegemeza na kubadilisha maisha. Haiwezekani kuwasha mtu mwingine ikiwa makaa yetu wenyewe yanafuka na kutoa moshi. Je, unaamini kwamba Yesu ndiye Masihi, kwamba alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, na kwamba alifufuka tena siku ya tatu? Je, unaamini kwamba alipaa mbinguni na hivi karibuni atarudi katika uwezo na utukufu ili kumaliza kazi aliyoianza karne nyingi zilizopita? Je, habari hizi zimeuteka moyo wako na shauku zako kiasi kwamba uko tayari kujidhabihu na kutoa dhabihu yoyote inayohitajika ili kuziona zikitangazwa hadi miisho ya dunia? Iwapo uko tayari kuzipokea kwa njia hii, utajiunga na msafara usiozuilika wa mitume, na kupanua ushawishi wa maisha yao hadi nyumbani kwako, mahali pa kazi, na kwa majirani zako. Ni maono kama haya tu jumuishi na yenye kuteka fahamu yatakayowapa wanafunzi wa mijini wa kizazi hiki maono ambayo wanaweza kuishi na kufa kwayo. Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Mungu wa Milele, kwa kumfufua Yesu katika wafu ulitangaza ushindi wake, na kwa kupaa kwake, ulimtangaza kuwa Bwana wa wote. Inua mioyo yetu mbinguni ambako anaishi na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja, sasa na hata milele. Amina. ~ Presbyterian Church (U.S.A.) na Cumberland Presbyterian Church. Kitengo cha Huduma ya Theolojia na Ibada. Kitabu cha Ibada ya Pamoja . Louisville, Ky: Westminister/John Knox Press, 1993. p. 333

Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi

4

Weka mbali vitabu na madokezo yako, kusanya mawazo na tafakari zako, na ujibu maswali ya jaribio la somo la 3, Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alikufa.

Jaribio

Fanya mazoezi pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu kwa kutamka andiko la kukumbuka ulilopewa kipindi kilichopita: 1 Petro 2:21-24.

Mazoezi ya kukariri maandiko

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walikusudia kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za kukusanya

Made with FlippingBook - Share PDF online