Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

1 5 2 /

M U N G U M W A N A

3. Tunapaswa kuelewaje kukawia kunakoonekana kwa kuja kwa Kristo – kwa nini muda mwingi umepita tangu ufufuo na kupaa? Mtazamo wetu wa sasa unapaswa kuwaje tunapongojea ujio wa Bwana? 4. Maandiko yanaelezeaje kazi ya kiungu ya hukumu, yaani, ni mshiriki gani wa Utatu ambaye amepewa heshima hii? 5. Ni vigezo gani ambavyo Hakimu Mwadilifu atatumia anapotoa hukumu juu ya wanadamu wote? 6. Ni thawabu gani itakayotolewa kwa waamini wanapohukumiwa kuhusiana na utumishi wao wa uaminifu kwa Bwana? Orodhesha “taji” mbalimbali zinazotajwa katika Agano Jipya zinazohusiana na kiti cha hukumu cha Kristo na thawabu ya waaminio. 7. Ipi itakuwa hatima ya wale ambao majina yao hayatakuwa yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo? Je! kuna tofauti gani kubwa kati ya hukumu ya Hakimu kwa waamini na hukumu yake kwa wasioamini? 8. Ufalme wa Yesu kama Bwana aliyeinuliwa utakuwa wa kimataifa na wa ulimwenguni pote katika maana gani? Taja Maandiko. Je, watakatifu wa Mungu watakuwa na hadhi gani katika Ufalme wa milele wa Kristo? 9. Katika ufunuo wa mji mpya, Yerusalemu Mpya, makao ya Mungu na Kristo yatahusianaje na watakatifu? Watachukua jukumu gani katika enzi mpya? 10. Kristo atafanya nini na Ufalme mara tu maadui wote watakapotiishwa chini ya miguu yake? Je, Mungu atakuwa na nafasi gani katika umilele ujao? Somo hili linaangazia kuinuliwa kwa Kristo katika ufufuo na kupaa, pamoja na kauli tatu za mwisho za sehemu ya Kristolojia ya Kanuni ya Imani ya Nikea ambayo inashuhudia juu ya kuja kwa Kristo katika utukufu, hukumu yake kwa wanadamu, na utawala wake ujao wa milele. Dhana zilizoorodheshwa hapa chini zinaangazia baadhi ya masuala muhimu na kweli zinazohusishwa na Kristo aliyeinuliwa, na kazi atakayokamilisha duniani katika nyakati zinazokuja. ³ Vipengele na maana mbali mbali za kuinuliwa kwa Kristo vinaweza kueleweka kwa uwazi kwa msingi wa matukio mawili muhimu ya wokovu; Kufufuka na Kupaa kwa Kristo.

4

MUUNGANIKO

Muhtasari wa Dhana Muhimu

ukurasa 295  7

Made with FlippingBook - Share PDF online