Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 1 5 5
M U N G U M W A N A
kuu ya miaka saba, na kisha, Kuja kwa Pili halisi, ambapo Kristo atatokea katika utukufu kamili, akihukumu mfumo mwovu wa ulimwengu, na kuusimika Ufalme wake juu yake. (Mtazamo huu ni maarufu katika mfululizo wa sasa wa Left Behind wa Timothy LaHaye). Kuhusiana na Ujio wa Pili wa Kristo, ni nini muhimu kwetu kuamini? Kwa mfano, je, ni lazima tuchukue msimamo fulani juu ya mtiririko mahususi wa matukio ya kuja kwake, au inatosha tu kukiri kwa moyo wote kwamba Ujio wa Pili utatokea? Njia nyingine ya kuuliza swali hili ni hii: Je, uthibitisho rahisi wa Kanuni ya Imani kwamba atakuja tena katika utukufu unatoa taarifa chache sana kuweza kweli kuhimiza mioyo ya Wakristo wanaongoja kurudi kwa Kristo? Tetea jibu lako kwa Maandiko. Katika mfululizo wa mafundisho kanisani juu ya Ujio wa Pili wa Kristo, mjadala mkali umekuwa ukiendelea miongoni mwa waalimu kadhaa wakubwa kanisani. Mmoja wa viongozi, aliyeathiriwa sana na mafundisho yanayotetea kwamba Ufalme wa Milenia wa Ufunuo 20 ni Ufalme halisi duniani ameanza mazungumzo na mmoja wa wafanyakazi wenzake ambaye anaamini kwamba Ufalme ni kama mfano tu wa utawala, si utawala halisi duniani. Wawili hawa ni watu wanaoheshimika, waliofunzwa vyema, watu wa Neno kweli kweli ambao wote wana moyo mzuri kwa ajili ya Bwana na wanatembea kwa kina na Mungu. Hata hivyo, mjadala wao umekuwa wa hadharani na mkali kiasi kwamba ni wazi kwamba kuna haja ya kuwepo kwa aina fulani ya utatuzi wa mazungumzo yao haraka iwezekanavyo. Uelewa wako wa “picha kuu” ya utawala wa Kristo unaokuja utakusaidiaje kusuluhisha mkanganyiko huku mahususi kuhusu kuja kwake? Vipengele mbalimbali na maana za kuinuliwa kwa Kristo vinaweza kueleweka kwa uwazi kwa msingi wa matukio mawili muhimu ya wokovu: kufufuka na kupaa kwa Kristo. Ufufuo unatumika kama uthibitisho wa Umasihi na uwana wa Yesu, na kupaa kwake kunampa Mwokozi wetu cheo cha hadhi na mamlaka kinachomruhusu kujaza vitu vyote kwa utukufu wake. Tukio la Kristo (yaani, kuwepo kwa Yesu kabla, maisha yake, huduma, kifo, ufufuo, na utukufu wake) linaweza kufikiriwa kwa maana ya mitazamo au mielekeo miwili, mwelekeo wa kushuka (katika unyonge au kunyenyekezwa), na kupanda (kuinuliwa). Kufufuka na kupaa vinahusishwa moja kwa moja na kuinuliwa kwa Kristo na utukufu wake. Kauli tatu mahususi katika Kanuni ya Imani ya Nikea zinazungumza juu ya kazi ya wakati ujao ya Yesu duniani . Kwanza, Kanuni ya Imani inazungumza kwamba Yesu Kristo atarudi tena katika utukufu, tendo ambalo litakuwa la ajabu kwa maana ya Hakutakuwa na Ufalme Halisi
3
4
Marejeo ya Tasnifu ya Somo
Made with FlippingBook - Share PDF online