Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 1 5 7
M U N G U M W A N A
Unapohitimisha masomo yako katika moduli hii, kuna masuala yoyote, watu, hali, au fursa zozote zinazohitaji kuombewa kama matokeo ya kujifunza kwako somo hili? Je, ni masuala gani hasa au watu ambao Mungu ameweka katika moyo wako kama matokeo ya somo hili ambao wanahitaji dua na maombi mahususi? Chukua muda wa kutafakari hili, na upokee msaada unaohitajika kwa njia ya ushauri na maombi kuhusiana na yale ambayo Roho amekuonyesha.
Ushauri na maombi
MAZOEZI
Hakuna maandiko ya kukariri katika somo hili.
Kukariri Maandiko
Hakuna kazi ya kukabidhi.
Kazi ya Usomaji
Kufikia sasa, unapaswa kuwa umeainisha na kufanyia maamuzi mapendekezo yako kuhusiana na Kazi ya Huduma na Kazi ya Eksejesia na kuyakabidhi kwa Mkufunzi wako ili ayapitie na kuyapitisha rasmi. Hakikisha kwamba unapangilia mapema muda wako na shughuli zako ili usichelewe kukamilisha kazi zako. Mwishoni kutakuwa na mtihani wa kufanyia nyumbani, na utajumuisha maswali yaliyochukuliwa kutoka kwenye majaribio matatu ya kwanza, maswali mapya kutoka kwenye maelezo ya somo hili, na maswali ya insha ambayo yatakutaka utoe majibu mafupi kwa maswali ya msingi yenye lengo la kuhusianisha somo na huduma na maisha. Pia, wakati wa mtihani, ni muhimu ujiandae kwa maswali ya kunukuu au kuandika mistari ya kukariri ya kozi hii. Utakapomaliza mtihani wako, tafadhali mjulishe mkufunzi wako na uhakikishe anapata nakala ya mtihani wako. Tafadhali zingatia: Ufaulu wako katika moduli hii hauwezi kupimwa na kujulikana kama hautafanya mtihani wa mwisho na kukusanya kazi zote na kuzikabidhi kwa mkufunzi wako (Fomu ya Ripoti ya Usomaji, kazi za kihuduma, kazi za ufafanuzi wa Maandiko, na mtihani wa mwisho). Katika somo hili la mwisho tumeangazia kwa kina matukio mawili kati ya matukio yanayoonyesha kuinuliwa kwa Kristo: ufufuo wake ambao unatumika kuthibitisha utambulisho wake kama Masihi na mwana wa Mungu, na kupaa kwake, ambako kunamweka Bwana wetu katika nafasi ya utukufu, uwakilishi wa kikuhani na ufalme. Bwana aliyefufuka na kuinuliwa atatawala na ni lazima atawale mpaka maadui wote wawekwe chini ya miguu yake. Kwa wakati wa Mungu mwenyewe,
Kazi Nyingine
ukurasa 296 9
Taarifa Kuhusu Mtihani wa Mwisho
4
Neno la Mwisho kuhusu Moduli hii
Made with FlippingBook - Share PDF online