Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

1 6 2 /

M U N G U M W A N A

K I A M B A T I S H O C H A 2 Tunasadiki: Tamko la Kanuni ya Imani ya Nikea (Mita ya kawaida) Mch. Dkt. Don L. Davis, 2007. Haki zote zimehifadhiwa. *Uimbo huu umetengenezwa kutoka katika ukiri wa Imani ya Nikea na umewekwa kwenye mita ya kawaida (8.7.8.6.), ikiwa na maana unaweza kuimbwa katika ala za hiyo hiyo, kama vile: Hata ndimi Elfu; Mwokozi Alinifia; Katika Neema ya Yesu; Jina la Yesu, Salamu; Damu imebubujika; Furaha kwa Ulimwengu.

Mungu Baba Mwenyezi anatawala, yeye aliyezifanya mbingu na nchi. Naam, Vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana, kwa yeye, viliumbwa na kwa yeye, vilitolewa.

Tuna amini katika Bwana mmoja, Yesu Kristo Mmoja, Mwana pekee wa Mungu, Aliyetolewa, sio kuumbwa, yeye na Bwana wetu ni wamoja!

Aliyetolewa toka kwa Baba, mwenye asili moja naye, Mungu na nuru; Kwa yeye vitu vyote viliumbwa na Mungu, katika yeye vitu vyote vilipewa uzima.

Yeye aliye kwa ajili yetu sote, kwa ajili ya wokovu wetu, alikuja hapa duniani kutoka mbinguni, akafanyika mwili kwa uweza wa Roho, na kwa kuzaliwa na Bikira mariamu

Ambaye kwa ajili yetu pia, alisulibiwa na utawala wa Pontio Pilato Akateseka, na akazikwa katika kaburi, lakini siku ya tatu, akafufuka.

Kama Maandiko Matakatifa yalivyosema, yote yaliyotokea yalikusudiwa kuwa hivyo. Akapaa juu mbinguni, katika mkono wa kuume wa Mungu, kwa sasa akikaa katika utukufu.

Naye atakuja tena katika utukufu kuwahukumu walio hai na wafu. Utawala wa ufalme wake hautakuwa na mwisho, kwa kuwa atatawala kama kichwa.

Tuna mwabudu Mungu, Roho Mtakatifu, Bwana wetu, na mtoaji wa uzima; Ametukuzwa pamoja na Baba na Mwana, Yeye ambaye amesema kwa njia ya manabii.

Na tuna amini katika Kanisa moja, watu watakatifu wa Mungu kwa nyakati zote, Katoliki kwa mipaka na mapana yake, lililojengwa katika msingi wa mitume!

Tukitambua ubatizo mmoja, kwa ajili ya msamaha wa dhambi zetu, Na tunatazamia siku ya ufufuo, kwa kuwa wafu wataishi tena.

Tukitazamia siku zisizokuwa na mwisho, maisha ya wakati ujao, Pale ambapo utawala mkuu wa Kristo utakuja duniani, mapenzi ya Mungu ndipo yatakapo fanyika!

Made with FlippingBook - Share PDF online