Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

1 7 8 /

M U N G U M W A N A

Mila (muendelezo)

5. Mtume Paulo kawaida anajumuisha umuhimu wa mapokeo katika kukazia utendaji wa fundisho lake. 1 Wakorintho 11.16 “Lakini mtu ye yote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.” (linganisha. 1 Kor. 1.2, 7.17, 15.3). 1 Wakorintho 14.33-34 “Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu. 34 Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.” 6. Mitume walipongeza pale ambapo kusanyiko linatumia mapokeo ili kubaki waaminifu kwenye “Neno la Mungu”. 1Wakorintho 11.2 “Basi nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vile vile kama nilivyowatolea.” 2 Wathesalonike 2.15 “Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu.” 2 Wathesalonike 3.6 “Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.”

Kiambatisho A

Waanzilishi wa Mapokeo: Ngazi Tatu za Mamlaka ya Kikristo

Kutoka 3.15 “Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.”

1. Mapokeo yenye Mamlaka: Mitume na Manabii (Maandiko Matakatifu)

Waefeso 2.19-21 Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. 20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. 21 Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. ~ Mtume Paulo

Made with FlippingBook - Share PDF online