Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
2 0 8 /
M U N G U M W A N A
K I A M B A T I S H O C H A 2 6 Mateso: Gharama ya Ufuasi na Uongozi wa Kiutumishi Don L. Davis
Kuwa mfuasi ni kubeba kuudhiwa na aibu ya yule aliyekuita katika utumishi (2 Tim. 3:12). Kwa kweli, hii inaweza kumaanisha kupoteza faraja, wepesi wa mambo, na hata maisha yenyewe (Yohana 12:24-25). Mitume wote wa Kristo walivumilia kutukanwa, kukemewa, kupigwa viboko, na kukataliwa na maadui wa Bwana wao. Kila mmoja wao alitia muhuri mafundisho yake kwa damu yake mwenyewe kupitia kukaa uhamishoni, mateso, na kifo cha kishahidi. Orodha hii hapa chini inaonyesha hatima za Mitume kulingana na maelezo ya kihistoria. • Mathayo aliuawa kwa upanga katika jiji la mbali la Ethiopia. • Marko alifia Aleksandria, baada ya kuburutwa kikatili katika mitaa ya jiji hilo. • Luka alitundikwa juu ya mzeituni katika nchi ya Ugiriki ya zamani. • Yohana aliwekwa katika chungu cha mafuta yanayochemka, lakini aliepuka kifo kwa njia ya kimuujiza, na baadaye akapigwa chapa huko Patmo. • Petro alisulubishwa huko Rumi na kichwa chake kikiwa chini. • Yakobo, aliye Mkuu zaidi, alikatwa kichwa huko Yerusalemu. • Yakobo, Mdogo, alitupwa kutoka kwenye kilele kirefu cha hekalu, na kisha kupigwa hadi kufa kwa rungu la dobi. • Bartholomayo alichunwa ngozi akiwa hai. • Andrea alifungwa msalabani, ambapo alihubiri kwa watesi wake hadi akafa. • Tomaso alichomwa mwili mzima kwa mikuki huko Coromandel huko East Indies. • Yuda aliuawa kwa kupigwa mishale. • Mathia alipigwa mawe kwanza na kisha kukatwa kichwa. • Barnaba wa Mataifa alipigwa mawe hadi kufa huko Salonika. • Paulo, baada ya mateso mbalimbali, hatimaye alikatwa kichwa huko Roma na Maliki Nero.
Made with FlippingBook - Share PDF online