Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 2 3 9

M U N G U M W A N A

Kiini na Chimbuko: Ukristo Ni Yesu Kristo (muendelezo)

B. Mpango wa Mungu ni kwamba Yesu awe wa kwanza, kichwa, kitovu, moyo wa yote anayozungumza na kufanya. Kumjua Mungu ni kumjua Kristo, kumpendeza Mungu ni kuwa kama Kristo, kumtii Mungu ni kufuata mfano wa Kristo: yeye ni kielelezo chetu. Yohana 13:13-16 - Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo. 14 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. 15 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo. 16 Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka. C. Maandiko kadhaa katika Agano Jipya yanaonyesha wazi kwamba kusudi la Mungu ni kutufananisha na sura halisi ya Yesu Kristo, kutuunganisha naye, na kisha kutufanya kama yeye. Mungu anakusudia kumfanya Yesu kuwa kichwa cha familia mpya ya kibinadamu ambayo itafananishwa na utu wake na hatima yake. • Rum. 8:28-29 - Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. 29 Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. • 1 Kor. 15:49 - Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni. • 2 Kor. 3:18 - Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho. • Paulo anaamuru katika Wafilipi 2:5: “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu.” • Katika Wafilipi 3:20, Paulo anasema kwamba uraia wetu uko mbinguni ambako tunamtazamia Bwana wetu, Kristo Yesu ambaye, kulingana na Wafilipi 3:21: “atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake”.

Made with FlippingBook - Share PDF online