Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 2 8 3
M U N G U M W A N A
Yesu, Masihi na Bwana wa Wote Ali kufa
MAELEZO YA MKUFUNZI 3
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi kwa ajili ya Somo la 3, Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alikufa . Lengo la somo hili ni kujaribu kuwasaidia wanafunzi kupata ufahamu wa kweli zinazohusiana na mateso na kifo cha Bwana wetu, pamoja na siri iliyomo katika mambo hayo. Hitaji hili la kufahamu maana ya kifo chake ni muhimu kwa yote ambayo somo hili litatafuta kufunua na kuwasilisha. Kitakachokuwa dhahiri kwako na kwa wanafunzi wako ni utofauti wa maoni kuhusu asili na maana ya kifo cha Kristo. Kilicho muhimu hapa ni kuona kwamba mikazo mbalimbali, ingawa ina vipengele vya ukweli, lazima ikataliwe au kueleweka katika mwanga wa mafundisho ya Maandiko yenyewe. Hili haipaswi kufanyika kwa nia ya kuhukumu na ya udhalili katika tathmini yetu ya aina mbalimbali za mitazamo ambayo imekuja kuhusishwa na mateso na kifo chake. Badala yake, ni kusema kwamba somo letu litazingatia zaidi maana zilizo wazi na zisizo na mkanganyiko tulizopewa na maandiko yenyewe ya Biblia kuhusu kifo cha Yesu. Unapopitia mitazamo mbalimbali pamoja na wanafunzi, itakuwa muhimu ukae karibu iwezekanavyo na mkazo wa Agano Jipya wa kifo cha Kristo, hasa kwa namna ambavyo katika mtazamo wa wokovu linavyojikita zaidi katika kifo chake kama mbadala kwa niaba ya wenye dhambi (ambao pia huitwa vicarious , ikimaanisha “mahali pa mwingine”). Maandiko kama vile Isaya 53, 1Timotheo 2:6, na 1 Petro 2:24 yanasisitiza aina hii ya mtazamo juu ya kifo cha Kristo kama kifo kwa ajili yetu , kwa niaba yetu (ona pia 2 Wakorintho 5:21; 1Petro 3:18 ikisisitiza kifo chake kwa niaba ya wanadamu wote). Hakikisha kwamba mkazo wako mwenyewe unaendana na ule wa mitume, ambao wana mwelekeo wa kukataa mtazamo wa kimonolitiki kuhusu maana ya kifo cha Yesu. Kwa mfano, kifo cha Yesu kimeleta ukombozi; tumenunuliwa kwa thamani, tulinunuliwa kutoka soko la watumwa la Shetani na dhambi ili tuishi tukiwa huru kama watumishi wa Mungu (2 Kor. 6:20 na 1 Kor. 7:23; Gal. 3:13; 4:5; Ufu. 5:9; 14:3-4). Zaidi ya hayo, tumepatanishwa na Mungu, tukirejeshwa kutoka katika hali ya kufarakana na kutengwa tuliyokuwa nayo kati yetu na Yeye kutokana na uasi wetu wa hiari dhidi ya mapenzi yake (Rum. 5:10; 2 Kor. 5:18-21). Kifo chake pia kilitupatia upatanisho mbele za Bwana, kikitosheleza madai yote ya Mungu wetu mtakatifu na kufanya njia ya ghadhabu yake ya kimungu kutoshelezwa na huruma yake kumwagika hata juu ya Mataifa yenye hatia (Rum. 3). Kwa kifo chake tumesamehewa dhambi zetu (Kol. 2:13) na dhambi zetu zilitupwa mbali
1 Ukurasa 85 Utangulizi wa Somo
Made with FlippingBook - Share PDF online