Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 2 8 5

M U N G U M W A N A

Tafakari ya aina hii mara moja inafunua kusudi halisi la ujuzi wa Kristolojia: ibada na upendo wa Mungu wetu mkuu na Baba, kwa njia ya Yesu Kristo. Upendo wa Mungu usiopimika, wa milele na wa ajabu ulionyeshwa kwa kupigwa kikatili, kupigwa mijeledi, kufedheheshwa, na hatimaye kifo cha kutisha cha Bwana wetu msalabani. Ajabu ya upendo wa Mungu haipaswi tu kusababisha uandishi wa insha zinazong’aa kwenye karatasi nyeupe, bali roho zilizovunjika, zilizonyenyekezwa mbele za Mungu na tayari kutumika kwa njia ile ile ambayo Bwana wetu mpendwa alijinyenyekeza na kuwa mtiifu hadi kifo, naam, kifo cha msalaba. Jaribu kuweka wazi hisia za kina na lugha ya moyo hapa, na sio tu katika ibada hii, lakini katika somo zima. Wawezeshe wanafunzi wako kuona na kuhisi onyesho la kutisha lilivyokuwa wakati Bwana wetu mpendwa alipojiweka mahali petu kubeba maovu na uasi ambao tumedhihirisha pasipo kujali na kwa upumbavu tangu utotoni. Hakika Bwana wetu alikufa kwa sababu Baba alichukua juu yake maovu yetu sisi sote . Mifano ya rejea katika somo hili imewekwa ili kusaidia kukazia ufahamu wetu kuhusu ukweli na maana za kifo cha Kristo. Hili ni mojawapo ya kazi muhimu zaidi, na ngumu hata hivyo, kwetu kama watu tunaolea na kukuza viongozi. Je, ni kwa namna gani na kwa njia zipi tunawasaidia viongozi wa Kikristo wanaoinukia kugundua tena maana ya kifo cha Yesu, wakati katika mazingira mengi sana kifo hicho kimepuuzwa, kimechukuliwa kidhahania kupita kiasi, na kwa hakika kupunguzwa umuhimu wake kama kiini cha imani na maisha ya Kikristo, katika suala la kazi yake ya msingi , iliyoleta wokovu na ukombozi wetu, na kazi yake ya kibinafsi , yaani, wajibu wetu wa kuchukua msalaba wetu na kumfuata, tukifananishwa na kifo chake ? Unapoendelea katika somo hili, kuwa mwangalifu hasa wa janga la siku hizi la aina ya ufahamu usio makini (badala ya ufahamu makini) wa kifo cha Yesu. Lengo letu lazima liwe kusaidia kutambulisha tena Kweli hii muhimu kwa uwazi na upya, ili wanafunzi wetu waweze kuona taswira ya Bwana kama aliyesulubiwa mbele yao. Paulo anaonyesha kwamba hili linawezekana katika ukosoaji wake wa ugonjwa wa Galatia wa kupuuza maana kubwa ya kifo cha Kristo kwa ajili ya wokovu na

 3 Ukurasa 88 Mifano ya rejea

Made with FlippingBook - Share PDF online