Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 5 1

M U N G U M W A N A

MIFANO YA REJEA

Je, Yesu alikuwa na uwezo wa kutenda dhambi?

Katika darasa la Shule ya Jumapili ya watu wazima, wakati wa mjadala kuhusu ubinadamuwaYesu, ilionekanawazi kwambamjadalahuoulighubikwanamabishano na mkanganyiko mkubwa kuhusu uwezo au kutoweza kwa Yesu kutenda dhambi kama mwanadamu. Wale waliosema kwamba inawezekana walijenga hoja kwamba, kwa kuzingatia aya nyingi zinazodokeza kwamba Yesu alikuwa kama sisi kwa kila namna isipokuwa tu hakutenda dhambi , ilimpasa awe na uwezo wa kutenda dhambi (kama kweli alikuwa kama sisi ). Wengine walikataa hoja hiyo wakisisitiza kwamba, kutokana na asili yake ya kiungu na takatifu, Yesu hangeweza kutenda dhambi kwa sababu alikuwa Mungu katika mwili , na kwa kuwa haiwezekani Mungu kutenda dhambi, hata Yesu (kama Mungu ) hangeweza kufanya dhambi. Je, ungejaribuje kusuluhisha mjadala wao juu ya swali hili muhimu la kitheolojia? Katika kujadili tangazo la Yesu la Ufalme uliopo ndani yake katika Marko 1:14-15 na maandiko mengine, baadhi ya wanafunzi waliuliza swali wakitaka kujua kama tafsiri hii ilikuwa na utetezi wenye maana ukizingatia matatizo halisi na hali ambazo ulimwengu unapitia . “Ikiwa Ufalme kwa namna fulani tayari umekuja katika Yesu Kristo, kwa nini basi mambo ni mabaya sana, kwa nini watu wengi wasio na hatia wanateseka ulimwenguni leo, na kwa nini hakomeshi uharibifu na ukatili wote duniani? ” Ikiwa kweli Ufalme ulizinduliwa kupitia tangazo la Yesu katika mahubiri yake huko Nazareti, basi kwa nini hatuoni ishara zaidi za kuwapo kwake katikati ya dunia ya leo ? Je, ungewezaje kujibu maswali haya na yanayofanana na hayo kuhusu Yesu kama Uzinduzi wa Ufalme na Mtangaza Ufalme wa Mungu katika enzi hii? Mengi ya mafundisho ya sasa yanaelekea kutumia aina fulani ya hemenetiki ya kuchagua kuhusiana na maana ya huduma ya Yesu kwetu kama Mtumishi wa Yehova anayeteseka. Kwa ujasiri na ushupavu, wainjilisti wengi wa kwenye runinga na watangazaji wa kidini wamebuni mpango wenye maelezo mazuri wa “afya na mali,” ambao unaelekea kufafanua Ukristo kama njia ya kupokea ustawi na baraka endapo watu watazingatia matumizi sahihi na endelevu ya “kanuni” za ustawi. Kwa njia nyingi, taswira za Yesu kama Mtumishi Atesekaye hubadilishwa na mawazo ya “ghala za baraka,” “kuendelea kukiri mpaka baraka zije,” na misemo inayohusiana na hayo, yote hayo yakilenga kumsaidia mtu kupata ujuzi wa kanuni za Mungu za baraka, na kuzitumia ili vipawa vya neema vitokanavyo na vinavyohusishwa na kanuni hizo viweze kujidhihirisha. Haionekani kama Ufalme upo Kichwa na sio mkia

1

2

2

3

Made with FlippingBook - Share PDF online