Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 5 3
M U N G U M W A N A
• Mafundisho mawili mashuhuri ya uzushi ya kihistoria ambayo yalipinga ubinadamu wa Yesu yaliwekwa wazi na kukanushwa katika mabaraza ya Kanisa la kwanza. Unestoria (Nestorianism) , fundisho kwamba Kristo alikuwa nafsi mbili tofauti , na Ueutikia (Eutychianism) , fundisho kwamba Kristo ana asili moja iliyochanganyika , yalikataliwa na kupingwa vikali kuwa ni uzushi kwa sababu ya namna yalivyokataa ubinadamu kamili wa Yesu. Mabaraza ya Nikea (325) na Chalcedon (381) yalisuluhisha maswali haya, yakithibitisha kwamba Yesu alikuwa Mungu kamili na mwanadamu kamili. • Mabaraza ya awali pia yalikanusha na kukataa makosa mengine muhimu yanayohusiana na kutafsiri vibaya ubinadamu wa Yesu: Docetism – uzushi ambao ulidai kwamba Yesu hakuwa mwanadamu na Apollinarianism ambao ulidai kwamba Yesu hakuwa mwanadamu kamili . • Mafundisho ya ubinadamu wa Kristo yamejaa athari nyingi na muhimu za kiutendaji zitokanazo na umoja wa asili ya kiungu na ya kibinadamu ya Yesu. Yesu akiwa kama sisi katika kila njia lakini bila dhambi na akiwa Kuhani Mkuu wetu, anaweza kuchukuliana nasi katika mahitaji yetu na kutuwakilishambele zaMungu. Kama Adamu wetu wa Pili, tutafananishwa na mwili wake wa utukufu wakati wa utukufu ujao. Sisi tunaoamini kwamba Mungu kweli aliishi duniani, na kuchukua hali ya chini ya umbo la mwanadamu, kwa kusudi la wokovu wa mwanadamu, tuko mbali sana na kufikiria kama wale wanaokataa kuamini kwamba Mungu anajali chochote.... Kwa bahati nzuri, hata hivyo, ni sehemu ya imani ya Wakristo kuamini kwamba Mungu alikufa, na bado kwamba yu hai milele. ~ Tertullian (c. 207, W), 3.319. David W. Bercot, ed. A Dictionary of Early Christian Beliefs . Peabody, MA: Hendrickson Publishers, 1998. p. 96.
“. . . Kristo alitimiza kikamilifu na kuunganisha katika nafsi yake nyuzi tatu kuu za matarajio ya Kimasihi ya Agano la Kale. Seremala wa Nazareti kwanza ni Nabii anayetangaza Neno la Bwana, kisha ni Kuhani anayeondoa dhambi kwa dhabihu na maombezi, na hatimaye ni Mfalme anayetawala juu ya ulimwengu wote. Mpango huu wenye sehemu tatu unatoa picha ya kazi ya upatanisho ambayo Bwana wetu alikuja duniani kuikamilisha.” ~ Bruce Demarest, Jesus Christ: The God-Man . Eugene, OR: Wipf and Stock Publishers, 1978. uk. 102.
2
I. Kusudi la Kuja kwa Mungu Mwana Duniani: Ufunuo na Ukombozi
Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video
A. Kwa habari ya Ufunuo
1. Yesu alitufunulia asili na nafsi ya Mungu .
Made with FlippingBook - Share PDF online