Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

8 2 /

M U N G U M W A N A

“Fomu ya Ripoti ya Usomaji” mwishoni mwa somo hili). Sasa ni wakati wa kuanza kupanga kuhusu kazi yako ya huduma kwa vitendo, na pia kuamua ni kifungu gani cha Maandiko utakachotumia kwa ajili ya kazi ya ufafanuzi wa Maandiko (eksejesia). Ni muhimu kwamba usichelewe au kuahirisha kuchagua maandalizi ya kazi yako ya huduma na ile ya eksejesia. Kadiri utakavyofanya maamuzi haraka kuhusu kile unachokusudia kufanya, ndivyo utakavyokuwa na muda wa kutosha kujiandaa na kufanya kazi zilizo bora zaidi. Katika somo hili tulichunguza ukamilifu wa asili ya kibinadamu ya Yesu, na umoja kati ya asili yake ya kiungu na ile ya kibinadamu. Yesu, ambaye alitungwa mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa na Bikira Maria, ndiye pekee mwenye asili mbili ambazo kila moja ni kamilifu, na ambaye asili yake ya kiungu na ya kibinadamu zimeunganishwa kikamilifu kuwa mtu mmoja. Pia tulizingatia mambo matatu makuu ya kibiblia ambayo yalijumuisha maisha ya Yesu na huduma yake ya Kimasihi duniani. Akiwa Yule Aliyebatizwa, Yesu alijihusisha na wenye dhambi aliokuja kuwakomboa. Kama Mtangaza Ufalme wa Mungu, Yesu alianzisha utawala wa Mungu na kuthibitisha tena haki ya Mungu ya kutawala uumbaji wake. Hatimaye, akiwa Mtumishi wa Yehova Atesekaye, Yesu alitimiza unabii wa Agano la Kale wa mtumishi wa Mungu aliyepakwa mafuta, akiwahubiria maskini Habari Njema, akitenda haki katikati ya watu, na kutoa uhai wake kuwa fidia ya wengi. Katika somo letu linalofuata lenye kichwa, Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alikufa , tutaangazia umaana wa kunyenyekezwa kwa Yesu Kristo, kwa maneno ya mwanatheolojia Oden, katika kujishusha kwake maishani na kujidhabihu kwake hata kufa kwa ajili ya ulimwengu.

Kuelekea Somo Linalofuata

2

Mtaala huu ni matokeo ya maelfu ya masaa ya kazi iliyofanywa na taasisi ya The Urban Ministry Institute (TUMI) na haupaswi kudurufu bila idhini ya taasisi hiyo. TUMI inatoa idhini kwa yeyote anayehitaji kutumia vitabu hivi kwa ajili ya faida ya ufalme wa Mungu, kwa kutoa leseni za kudurufu za gharama nafuu. Tafadhali thibitisha kwa Mkufunzi wako ikiwa kitabu hiki kimepewa leseni ipasavyo. Kwa taarifa zaidi kuhusu TUMI na taratibu zetu za utoaji leseni, tembelea www.tumi.org na www.tumi.org/license .

Made with FlippingBook - Share PDF online