Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 8 7
M U N G U M W A N A
Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote. ” Tukitazama kwa makini andiko hilo tunashangazwa na tabia na matendo ya watu dhidi yake. Alidharauliwa, alikataliwa, mtu wa huzuni, aliyejua masikitiko, asiyestahiwa na asiyependwa. Ingawa alionekana kwa kinaya kama mtu aliyepigwa na Bwana, kwa hakika alikuwa akibeba huzuni zetu, alijeruhiwa kwa ajili ya makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu, aliadhibiwa kwa ajili ya amani yetu, na kupigwa vikali kwa ajili ya uponyaji wetu. Sisi kama kondoo tumepotea na kuziendea njia zisizo na uhusiano wowote na Bwana, tumegeukia kila mtu njia yake mwenyewe, na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi sote. Ukweli huu, kwamba kunyenyekezwa kwake kulikuwa ni matokeo ya uasi na dhambi zetu, unapaswa kuleta ndani ya kila mmoja wetu hisia za kina za utulivu na huzuni. Nyimbo zimetupa ufunuo huu wa mielekeo ya aina hii katika kuutafakari msalaba wa ajabu, katika kuona kichwa kitakatifu kikijeruhiwa kwa sababu ya upumbavu na makosa yetu wenyewe. Upendo wa Bwana uliomsukuma kupatanisha, kukomboa na kurejesha ulimfanya kumwadhibu Mtumishi wake mwenyewe badala yetu, akiweka juu yake maovu yetu sisi sote . Hakuna ukweli mwingine wala hakuna wazo lingine linaloweza kuleta ndani yetu kiwango cha kina cha kujitambua kwa habari ya matokeo halisi ambayo dhambi yetu ilileta juu ya Bwana wetu. Mapigo, adhabu, kukataliwa, na kudharauliwa kwake kulisababishwa moja kwa moja na kutotii kwetu, uongo, tamaa, na ubinafsi wetu. Upotevu wetu na chuki zetu, maudhi yetu na husuda zetu na upumbavu wetu na matusi yetu ni sababu za mateso na kifo cha Bwana wetu. Tunapofikia kuelewa jinsi tunavyowajibika kwa mateso yake, ni hapo tu ndipo tutaweza kweli kumhurumia Bwana wetu, na kubeba kila siku msalaba ambao tunapaswa kushiriki pamoja naye. Ni lazima tukubali sehemu yetu pale Kalvari, mchango ule uliofanya kifo chake kuwa cha lazima kwa ajili ya ukombozi wetu . Ni kweli, tumekwenda katika njia zetu wenyewe; naam, tumepotea kama kondoo wanaopotea wasio na mchungaji, na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi sote.
3
Made with FlippingBook - Share PDF online