Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 8 9

M U N G U M W A N A

Mateso ya Kristo

Kakitka kuitikia kwa habari ya filamu maarufu zaidi ya Mateso ya Yesu (The Passion of the Christ) , makanisa mengi ya Kiinjili yalifanya mikutano ya kiinjilisti iliyobuniwa kwa kusudi la kutangaza Habari Njema sambamba na uingizwaji wa filamu hiyo sokoni. Hali ya picha ya mateso ya Masihi iliyoonyeshwa katika filamu ile imesababisha mwitikio wa aina tofauti, kuanzia hisia za kina za majuto na upendo hadi mshtuko na hofu. Filamu hiyo labda ndio taswira ya ukatili wa kutisha zaidi kuwahi kuigizwa kuhusiana na mateso ya Yesu. Wengine wamesema maonyesho kama haya yameenda mbali mno katika kuangazia ukatili wa Kalvari bila kufunua kwa kiasi kikubwa sababu za msingi za ukatili huo. Je, una maoni gani kuhusu tafsiri hizo za ajabu za mateso ya Yesu. Je, tunapaswa kutoa zaidi ya hizi, au tumezipata za kutosha kwa sasa? Katika makanisa yetu mengi yanayozingatia zaidi kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya «watafutaji», tunashuhudia ukimya wa ajabu kwa habari ya unyanyapaa na mateso ya Kalvari. Mengi ya mahubiri na homilia ni kuhusiana hasa na mada zinazovutia watu wengi, na kwa kawaida yanaepuka mada na jumbe ambazo zina mkazo mkubwa wa kitheolojia na mafundisho ya kidini. Msalaba unapozungumziwa, kwa kawaida huzungumziwa kwa namna inayomafanya msikilizaji ajisikie kuwa ana uwezo na ni wa thamani badala ya kuwa suluhisho la wazi la uasi wa wanadamu. Nafasi ya mafundisho hukusu dhabihu ya damu ya Masihi imechukuliwa na mahubiri juu ya mawazo chanya na kujenga kumbukumbu za familia. Nafasi ya nyimbo nyingi za zamani ambazo zilizungumzia ajabu, nguvu, na siri ya msalaba imechukuliwa na mafuriko ya pambio ambazo zote zinalenga furaha ya mwabudu na sio mateso ya msingi ambayo yalifanya ibada iwezekane. Ingawa makanisa mengi yanaendelea kusisitiza msalaba kama tukio kuu katika historia ya wokovu, mbinu zetu za uinjilisti na uenezaji wa Habari Njema zinalenga zaidi mada chanya kwa ajili ya kuvutia wageni wapya. Je, una maoni gani kuhusu kuongezeka kwa ukimya huu wa kustaajabisha kuhusiana na msalaba katika mahubiri, mafundisho na ibada za makanisa yetu leo? Kimya cha ajabu

2

3

3

Made with FlippingBook - Share PDF online