Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

Jiwe Walilolikataa Waashi Limekuwa Jiwe Kuu la Pembeni

Mungu Roho Mtakatifu

THE UR BAN

MI N I S T R Y I NS T I TUT E h u d uma y a WOR L D IMPAC T , I NC .

u

b

c

a

h

i t

a

K

M

i

z

w

n

a

u

f

n

a

Moduli ya 14 Theolojia & Maadili

SWAHILI

K I T A B U C H A M W A N A F U N Z I

Mungu Roho Mtakatifu

Moduli ya 14

Theolojia na Maadili

Nafsi ya Roho Mtakatifu

Kazi ya Kinabii ya Roho Mtakatifu

Uwepo wenye Nguvu wa Roho Mtakatifu – sehemu ya I

Uwepo wenye Nguvu wa Roho Mtakatifu – sehemu ya II

Mtaala huu ni matokeo ya maelfu ya masaa ya kazi iliyofanywa na taasisi ya The Urban Ministry Institute (TUMI) na haupaswi kudurufu bila idhini ya taasisi hiyo. TUMI inatoa idhini kwa yeyote anayehitaji kutumia vitabu hivi kwa ajili ya faida ya ufalme wa Mungu, kwa kutoa leseni za kudurufu za gharama nafuu. Tafadhali thibitisha kwa Mkufunzi wako ikiwa kitabu hiki kimepewa leseni ipasavyo. Kwa taarifa zaidi kuhusu TUMI na taratibu zetu za utoaji leseni, tembelea www.tumi.org na www.tumi.org/license .

Moduli ya 14 ya Capstone: Mungu Roho Mtakatifu – Kitabu cha Mwanafunzi ISBN: 978-1-62932-367-1 © 2005, 2011, 2013, 2015. Taasisi ya The Urban Ministry Institute . Haki zote zimehifadhiwa. Toleo la Kwanza 2005, Toleo la Pili 2011, Toleo la Tatu 2013, Toleo la Nne 2015. © 2023 Toleo la Kiswahili, kimetafsiriwa na Robin Mwenda na Eresh Tchakubuta. Hairuhusiwi kunakili, kusambaza na/au kuuza vitabu hivi, au matumizi mengine yoyote pasipo idhini, isipokuwa kwa matumizi yanayo ruhusiwa kwa mujibu wa sheria ya Haki Miliki ya Mwaka 1976 au kwa idhini ya maandishi kutoka kwa mmiliki. Maombi ya idhini yatumwe katika maandishi kwa taasisi ya: The Urban Ministry Institute , 3701 E. 13th Street, Wichita, KS 67208. Taasisi ya The Urban Ministry Institute ni huduma ya World Impact, Inc Nukuu zote za Maandiko, isipokuwa kama imeonyeshwa vinginevyo, zimechukuliwa kutoka katika SWAHILI BIBLE UV050(MCR) series® Haki Miliki © 1997, iliyochapishwa na The Bible Society of Tanzania . Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote za kimataifa zimehifadhiwa.

Yaliyomo

Muhtasari wa kozi

3 5 7

Kuhusu Mkufunzi

Utangulizi wa Moduli

Mahitaji ya Kozi

15

Somo la 1 Nafsi ya Roho Mtakatifu

1

51

Somo la 2 Kazi ya Kinabii ya Roho Mtakatifu

2

81

Somo la 3 Uwepo wenye Nguvu wa Roho Mtakatifu – sehemu ya I

3

117

Somo la 4 Uwepo Wenye Nguvu wa Roho Mtakatifu – sehemu ya II

4

151

Viambatisho

/ 3

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Kuhusu Mkufunzi

Terry Cornett (B.S., M. A., M.A.R.) ni Mwalimu wa Taaluma wa Heshima (Dean Emeritus) katika Taasisi ya The Urban Ministry huko Wichita, Kansas. Ana Shahada kadhaa kutoka katika Chuo Kikuu cha Texas huko Austin, Chuo cha Wheaton Graduate School, na Chuo cha Theolojia cha C. P. Haggard katika Chuo Kikuu cha Azusa Pacific. Terry alihudumu kwa miaka 23 kama mmishenari wa maeneo ya mijini wa World Impact kabla ya kustaafu mwaka 2005. Katika kipindi hicho alihudumu Omaha, Los Angeles, na Wichita ambako alihusika katika huduma za upandaji makanisa, elimu, na mafunzo ya uongozi.

/ 5

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Utangulizi wa Moduli

Salamu katika Jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu! Kuna kweli chache za kitheolojia katika historia ya Kanisa ambazo zimezua mabishano mengi, kutokubaliana, na mafarakano kama fundisho la Roho Mtakatifu. Kuanzia mabishano ya zamani kuhusu Utatu na fundisho la “ procession ” (yaani fundisho kuhusu nafsi ipi ya Utatu iliipeleka nafsi nyingine kutenda kazi) hadi kutokubaliana kwa siku za leo kuhusiana na ubatizo na karama za Roho Mtakatifu, kuna mengi ambayo yanaweza kutufanya tuliendee somo hili kwa tahadhari; lakini, ninatumai kwa dhati kwamba haitakuwa hivyo. Fundisho la Roho Mtakatifu ni kiini cha uelewa wetu kuhusu asili ya Mungu na namna tunavyoweza kuuishi uwepo wake hai katikati yetu. Roho ametumwa ili kulitia nguvu na kuliongoza Kanisa la Mungu na kuwapa maisha mapya wale wote wanaoitikia kwa imani ujumbe wake kuhusu Yesu. Ni imani yetu kwamba ukweli unaojifunza kuhusu Roho Mtakatifu hautakuwa tu “theolojia rasmi” ambayo inakusaidia kumwelewa Mungu vizuri zaidi, lakini pia itakuwa “theolojia ya vitendo” ambayo inakuwezesha kumtegemea Roho Mtakatifu katika kiwango kinachoongezeka daima kwa kadri unavyoendelea kuhudumu katika Kanisa la Mungu na kushuhudia ulimwenguni. Somo la kwanza, Nafsi ya Roho Mtakatifu , linalenga kufundisha juu ya Mungu Roho kama nafsi ya tatu ya Mungu mmoja wa Utatu. Tutachunguza taswira ya kibiblia ya Roho kama nafsi ya kiungu ambayo ni Mungu na ambayo inatenda kazi katika ufahamu wa kiungu kama Mungu. Pia tutazungumzia uhusiano wa Roho na Baba na Mwana, tukimtazama Roho kama “kifungo cha upendo” kati yao na “zawadi yao ya upendo kwa ulimwengu.” Tutazungumza kuhusu Roho kama “Mpaji wa Uhai” na kuonyesha jinsi majina, vyeo, na alama za Roho katika Maandiko zinavyomwonyesha yeye kama chanzo na mtegemezaji wa maisha ya kimwili na ya kiroho na kama nafsi iliyo kazini ili kuvifanya vitu vyote kuwa vipya. Katika somo letu la pili, Kazi ya Kinabii ya Roho Mtakatifu , tutachunguza asili ya ufunuo wa kinabii, jambo ambalo litatuleta katika ufahamu wa ukweli kwamba Roho ndiye anayelivuvia na kuliangazia Neno la Mungu. Pia tutaona kwamba jukumu la kinabii la Roho linajumuisha huduma yake ya kusadikisha. Yeye ndiye anayeushinda udanganyifu unaosababishwa na dhambi na kutuongoza kwenye toba ya kweli. Kazi ya unabii ya Roho Mtakatifu ni njia ambayo Mungu anajifunua kwetu na njia ambayo anatuwezesha kuamini ufunuo huo.

6 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Somo la tatu na la nne linahusu Uwepo Wenye Nguvu wa Roho Mtakatifu (Sehemu ya I) na Uwepo Wenye Nguvu wa Roho Mtakatifu (Sehemu ya II) . Hapa mkazo ni kile ambacho Roho Mtakatifu anafanya katika maisha ya wale wanaotubu na kuamini. Tutazungumza kuhusu jukumu la Roho katika kuzaliwa upya, kufanywa wana, ubatizo, karama, kukaa ndani ya waamini, kutia muhuri na utakaso. Tutakuja kuelewa kwamba kazi ya nguvu ya Roho huliwezesha Kanisa kutimiza utume wake ulimwenguni. Nafsi ya Roho Mtakatifu ni halisi na yenye umuhimu kama Mungu Baba na Mungu Mwana. Roho ametumwa na Baba na Mwana ulimwenguni ili tuweze kuwa na ushirika na Mungu, kupokea upendo wake na kudumu katika huo, na ili tuweze kutiwa nguvu katika kutii amri za Mungu na kutimiza kazi ya utume aliyotuitia. Ombi letu ni kwamba kiwango chako cha kumtegemea Roho kikue tunapojifunza Maandiko pamoja.

- Mchungaji Terry G. Cornett

/ 7

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Mahitaji ya Kozi

• Biblia (kwa madhumuni ya kozi hii, Biblia yako inapaswa kuwa tafsiri [mf. BHN, SUV, NEN, SRUV, au NIV, NASB, RSV, KJV, NKJV, n.k. ikiwa utatumia Biblia ya Kiingereza], na sio Biblia iliyofafanuliwa [mf. The Living Lible, The Message ]). • Kilamoduli katikamtaalawaCapstone imeainishavitabuvyakiada ambavyo vinatakiwa visomwe na kujadiliwa katika muda wote wa kujifunza moduli husika. Tunakuhimiza kusoma, kutafakari, na kufanya kazi husika pamoja na wakufunzi wako, wasimamizi, na wanafunzi wenzako. Kutokana na uhaba wa vitabu unaoweza kujitokeza kwa sababu kadha wa kadha (k.m., kushindwa kuchapisha vitabu vya kutosha), tunaweka orodha yetu ya vitabu rasmi vya Capstone vinavyohitajika kwenye tovuti yetu. Tafadhali tembelea www.tumi.org/books ili kupata orodha ya vitabu vinavyohitajika kwa ajili ya moduli hii. • Daftari na kalamu kwa ajili ya kuchukua maelezo na kufanyia kazi za darasani.

Vitabu na nyenzo zingine zinazohitajika

• Fee, Gordon D. Paul, the Spirit, and the People of God. Peabody, MA: Hendrickson, 1996.

Vitabu vya kusoma

• The Trinity Pamphlet. Torrance, CA: Rose Publishing, Inc., 2005 (www.rose-publishing.com).

Vitabu kwa ajili ya rejea

8 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Muhtasari wa mfumo wa kutunuku matokeo na uzito wa gredi.

Mahitaji ya Kozi

Mahudhurio na ushiriki darasani . . . . . . . 30% Mazoezi . . . . . . . . . . . . . . . . . 10% Mistari ya Kukumbuka . . . . . . . . . . . 15% Kazi za ufafanuzi wa Maandiko. . . . . . . . 15% Kazi za huduma. . . . . . . . . . . . . . 10% Usomaji na kazi za kufanyia nyumbani . . . . . 10% Mtihani wa mwisho. . . . . . . . . . . . . 10%

alama 90 alama 30 alama 45 alama 45 alama 30 alama 30

alama 30 Jumla: 100% alama 300

Mambo ya kuzingatia katika utoaji maksi

Kuhudhuria kila kipindi ni moja ya masharti ya msingi ya kozi hizi. Kukosa kipindi kutaathiri matokeo yako. Ikiwa una dharura isiyoepukika itakayokulazimu kukosa kipindi, tafadhali mjulishe mkufunzi wako mapema. Ukikosa kipindi ni jukumu lako kutafuta taarifa kuhusu kazi na mazoezi yaliyotolewa, na kuongea na mkufunzi wako pale inapobidi kufanya na kukabidhi kazi kwa kuchelewa. Sehemu kubwa ya mafunzo yanayohusiana na kozi hii hufanyika kupitia mijadala. Kwa hivyo, unahimizwa na kutarajiwa kushiriki kikamilifu katika kila kipindi cha kozi hii. Kila kipindi kitaanza na jaribio fupi kuhusu mawazo ya msingi yaliyofundishwa katika somo lililopita. Njia nzuri zaidi ya kujiandaa na majaribio haya ni kupitia Kitabu cha Mwanafunzi na daftari uliloandikia maelezo ya somo hilo lililopita. Kukariri Neno la Mungu ni kipaumbele cha msingi kwa maisha na huduma yako kama mwamini na kiongozi katika Kanisa la Yesu Kristo. Kozi hii ina mistari ya Biblia michache, lakini yenye umuhimu mkubwa katika jumbe zake. Katika kila kipindi utahitajika kukariri na kunukuu (kwa mdomo au kuandika) mistari ya Biblia uliyopewa na mkufunzi wako. Neno la Mungu ni zana yenye nguvu ambayo Mungu anaitumia ili kuwaandaa watumishi wake kwa kila kazi ya huduma aliyowaitia (2 Tim. 3:16-17). Ili kutimiza matakwa ya kozi hii, lazima uchague kifungu cha Biblia na kufanya uchambuzi wa kina (yaani, ufafanuzi wa Maandiko). Kazi yako iwe na kurasa tano ziliyochapwa kwa kuacha nafasi mbili kati ya mistari au kuandikwa vizuri kwa mkono, na ielezee kile tunachoweza kujifunza kwa kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu kupitia andiko hili. Ni shauku na matumaini yetu kwamba utashawishika kikamilifu na kuamini juu ya uwezo wa Maandiko kuleta badiliko na athari chanya katika maisha yako na ya wale unaowahudumia. Unapoendelea kujifunza kozi hii, uwe huru

Mahudhurio na ushiriki darasani

Majaribio

Kukariri mistari ya Biblia

Kazi za ufafanuzi wa Maandiko

/ 9

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

kuongeza mistari kadhaa katika uchambuzi wako (takriban mistari 4-9) kuhusu jambo ambalo ungependa kujifunza kwa kina. Maelezo yote kuhusiana na kazi hii yametolewa katika ukurasa wa 10-11, na yatajadiliwa katika sehemu ya utangulizi ya kozi hii. Matarajio yetu ni kwamba wanafunzi wote watatumia mafunzo haya kivitendo katika maisha yao na katika majukumu yao ya kihuduma. Mwanafunzi atakuwa na jukumu la kufikiria namna ya kufanya mafunzo ya huduma kwa vitendo kwa kutumia kanuni alizojifunza katika mazingira halisi ya huduma. Maelezo ya namna ya kufanya mafunzo kwa vitendo yanapatika katika ukurasa wa 12, na yatajadiliwa katika kipindi cha utangulizi wa kozi. Mkufunzi wako anaweza kutoa kazi za darasani na kazi za nyumbani za aina mbalimbali wakati wa vipindi vya masomo au anaweza kuziandika katika Kitabu chako cha Mwanafunzi. Ikiwa una swali lolote kuhusu kile kinachohitajika kuhusiana na kazi hizi au muda wa kuzikusanya, tafadhali muulize mkufunzi wako. Ni muhimu kwa kila mwanafunzi kusoma maeneo yote ambayo inampasa kusoma katika vitabu husika vya kozi hii au katika Maandiko Matakatifu ili kujiandaa kwa ajili ya mijadala darasani. Tafadhali hakikisha unajaza na kukabidhi kwa Mkufunzi wako “Jedwali la Tathimini ya Usomaji” lililomo katika Kitabu cha Mwanafunzi, kila wiki. Kutakuwa pia na fursa ya kupata alama za ziada endapo utasoma zaidi ya ulivyoagizwa. Mwishoni mwa kozi, Mkufunzi wako atakupa mtihani wa mwisho utakaofanyia nyumbani. Katika mtihani huu hautaruhusiwa kutumia vitabu vyako vya kozi hii isipokuwa Biblia. Utaulizwa swali ambalo litakusaidia kutafakari juu ya yale uliyojifunza katika kozi na namna yanavyoathiri mfumo wako wa fikra na utendaji wako katika huduma. Utakapokabidhiwa mtihani wa mwisho, mkufunzi wako atakupa taarifa zaidi kuhusu tarehe za kukamilisha na kukabidhi mtihani wako na kazi nyinginezo.

Kazi za huduma

Kazi za darasani na za nyumbani

Kazi za usomaji

Mtihani wa mwisho wa kufanyia nyumbani

Gredi za ufaulu

Mwishoni mwa kozi hii, gredi zifuatazo zitatolewa na kuhifadhiwa kwenye mbukumbu za kila mwanafunzi. A – Bora D – Inaridhisha B – Nzuri sana F – Hairidhishi (Feli) C – Nzuri I – Isiyokamilika

1 0 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Matokeo ya mwisho wa kozi yatatolewa katika mfumo wa gredi kwa kutumia skeli ya kutunuku matokeo kwa mtindo wa herufi zenye alama chanya na hasi, kisha alama za gedi yako ya ufaulu katika kazi mbali mbali zitajumlishwa na kugawanywa kwa idadi ya kazi na vipimo vingine husika ili kupata wastani wa matokeo yako ya mwisho. Kuchelewesha au kushindwa kabisa kukabidhi kazi zako kutaweza kuathiri matokeo yako. Hivyo, ni vyema kupangilia shughuli na muda wako mapema na kuwasiliana na mkufunzi wako endapo kutakuwa na changamoto yoyote. Kama sehemu ya ushiriki wako katika kusoma moduli ya Mungu Roho Mtakatifu , utahitajika kufanya kazi ya ufafanuzi wa Maandiko (uchunguzi wa ndani ya Maandiko yenyewe) kwa kutumia andiko mojawapo kati ya Maandiko yafuatayo kuhusiana na kazi ya Roho Mtakatifu:  Yohana 14:15-18  Warumi 8:1-27  1 Wakorintho 2:9-16  Yohana 16:7-11  Warumi 8.12-17  Wagalatia 4:4-7 Dhumuni la kazi hii ni kukupa fursa ya kufanya utafiti wa kina wa kifungu kinacholengwa zaidi cha Maandiko kuhusiana na kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa kutumia kifungu hicho kama msingi, fikiria kwa makini kuhusu njia ambazo Maandiko haya yanaweka wazi kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha ya mwamini, kanisa, na ulimwengu. Unaposoma sehemu hiyo, tumaini letu ni kwamba uchambuzi wako utaongeza ufahamu wako wa namna ambavyo Roho Mtakatifu anafanya kazi ili kukamilisha kusudi la Mungu Ulimwenguni. Vilevile tuna shauku kwamba Roho akupe ufahamu kuhusiana na namna ya kuhusianisha maana yake na safari yako binafsi kama mwanafunzi, pamoja na kazi ya uongozi ambayo Mungu amekupa katika kanisa na huduma yako. Hii ni kazi ya kujifunza Biblia, na ili kufanya kazi ya ufafanuzi, ni lazima udhamirie kuelewa maana ya andiko husika katika muktadha wake. Ukishajua andiko lilimaanisha nini kwa wasomaji wake wa kwanza, unaweza kupata kanuni zinazotuhusu sisi sote leo, na kuzihusianisha kanuni hizo na maisha. Mchakato wa hatua tatu rahisi unaweza kukuongoza katika jitihada zako binafsi za kujifunza kifungu cha Biblia: 1. Je, Mungu alikuwa akisema nini kwa watu katika muktadha wa asili wa andiko husika? 2. Ni kanuni gani ambazo andiko hili linafundisha ambazo ni kweli kwa watu wote kila mahali, ikiwa ni pamoja na sisi leo ? Kazi za ufafanuzi wa Maandiko

Dhumuni

Mpangilio na muundo

/ 1 1

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

3. Ni kitu gani Roho Mtakatifu ananiagiza kufanya kupitia kanuni hii, leo, katika maisha na huduma yangu ? Baada ya kuwa umeyajibu maswali haya katika kujifunza kwako kibinafsi, hapo sasa utakuwa tayari kuendelea kuandika ulichokigundua katika kazi uliyopewa . Angali hapa chini mfano wa muhtasari wa kazi yako: 1. Eleza kile unachoamini kuwa ndio mada kuu au wazo kuu la andiko ulilochagua. 2. Eleza kwa muhtasari maana ya andiko hilo (unaweza kufanya hivi katika aya mbili au tatu, au, ukipenda, kwa kuandika ufafanuzi mfupi wa mstari kwa mstari juu ya kifungu husika). 3. Eleza kanuni kuu moja hadi tatu au maarifa ambayo kifungu hiki kinatoa kuhusu kazi ya RohoMtakatifu na jinsi Wakristo wanapaswa kuitikia kwake. 4. Eleza jinsi kanuni moja, kadhaa, au zote zinaweza kuhusiana na yafuatayo: Kwa msaada au mwongozo, tafadhali uwe huru kusoma vitabu vya rejea vya kozi hii na/au vitabu vya mafafanuzi (commentaries), na kutumia maarifa yaliyomo katika vyanzo hivyo katika kazi yako. Unapotumia maarifa au mawazo ya mtu mwingine kujenga hoja zako, hakikisha unatambua kazi za waandishi husika kwa kutaja vyanzo vya taarifa hizo. Astahiliye heshima apewe heshima yake. Tumia marejeleo ya ndani ya maandishi ( in-text-refences ), tanbihi ( footnotes ), au maelezo ya mwisho ( endnotes ). Njia yoyote utakayochagua kutaja rejea zako itakubalika, ilimradi 1) utumie njia hiyo moja katika kazi nzima, na 2) uonyeshe pale unatumia mawazo ya mtu mwingine, na umtambue mwandishi husika kwa kumtaja. (Kwa maelezo zaidi, angalia katika Kiambatisho cha Namna ya Kuandika Kazi Yako: Mwongozo wa Kukusaidia Kutambua Waandishi wa Vitabu vya Rejea .) Kabla hujakabidhi kazi yako, hakikisha inasifa zifuatazo: • Imeandikwa au kuchapwa vizuri na inasomeka na kueleweka. a. Kiroho chako binafsi na namna unavyotembea na Kristo b. Maisha na huduma yako katika kanisa lako la mahali pamoja c. Hali au changamoto katika jamii yako kwa ujumla.

• Ni uchambuzi wa mojawapo ya vifungu hapo juu. • Imekusanywa kwa wakati (haijacheleweshwa). • Ina urefu wa kurasa 5.

1 2 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

• Inafuata muhtasari au mpangilio uliotolewa hapo juu, na imeandikwa kwa namna ambayo msomaji ataweza kuelewa. • Inaonyesha jinsi kifungu husika kinavyohusiana na maisha na huduma leo. Usiruhusumaagizo haya yakuogopeshe; hii ni kazi ya kujifunza Biblia! Unachohitaji kuonyesha katika kazi hii ni kwamba ulisoma andiko husika, umeeleza kwa muhtasari maana yake, ukaweza kupata kanuni chache muhimu kutoka katika andiko hilo, na kuzihusianisha na maisha na huduma yako mwenyewe. Kazi ya ufafanuzi inabeba alama 45 na inawakilisha 15% ya jumla ya maksi zako, hivyo hakikisha kwamba unaifanya kazi yako kuwa bora na yenye maarifa ya kutosha ya Neno la Mungu. Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo (Waebrania 4:12). Mtume Yakobo anaweka msisitizo zaidi juu ya kuwa watendaji wa Neno la Mungu, sio wasikiaji tu, tukijidanganya wenyewe. Tunahimizwa kulifanyia kazi, kulitii. Anaongeza kusema kwamba kupuuza nidhamu hii ni sawa na sisi kujitazama sura zetu za asili katika kioo na mara tunapoondoka tunasahau asili yetu (sis ni nani) na tulichokusudiwa kuwa. Katika kila hali, mtendaji wa Neno la Mungu atabarikiwa katika kila afanyacho (Yakobo 1:22-25). Shauku yetu ya dhati ni kwamba uweze kutumia maarifa unayojifunza kwa vitendo, ukihusianisha elimu hii na masuala na mahitaji halisi katika maisha yako binafsi, na huduma yako ndani ya kanisa lako na kupitia kanisa lako. Kwa sababu hiyo, kama takwa mojawapo muhimu la kukamilisha moduli hii, utatakiwa kufikiria namna ya kufanya mafunzo ya huduma kwa vitendo ambapo utaweza kuwashirikisha wengine sehemu ya maarifa ambayo umejifunza katika kozi hii. Kuna njia nyingi ambazo unaweza kutumia kutimiza takwa hili la kujifunza kwako. Unaweza kuchagua kuwa na muda wa kujifunza na mtu binafsi, kutumia madarasa ya Shule ya Jumapili, vikundi vya vijana au watu wazima, au hata kwa kupata nafasi ya kuhudumu mahali fulani. Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unajadili na hadhira baadhi ya maarifa uliyojifunza kutoka darasani. (Bila shaka, unaweza kuchagua kuwashirikisha nao baadhi ya maarifa toka katika kazi yako ya Ufafanuzi wa Maandiko ya moduli hii). Uwe huru na tayari kubadilika na kuendana na mazingira yoyote unapofanya kazi yako. Ifanye iwe yenye ubunifu na inayoruhusu kusikiliza mitazamo tofauti kwa Kazi ya huduma

Utoaji maksi

Dhumuni

Mpangilio na muundo

/ 1 3

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

nia ya kujifunza. Fanya uchaguzi mapema kabisa kuhusu aina ya muktadha ambao unatamani kutumia kushirikisha watu wengine maarifa haya na kisha mshirikishe Mkufunzi wako juu ya maamuzi hayo. Panga hayo yote mapema na epuka kusubiri dakika za mwisho kuamua na kutekeleza kile unachotaka katika kazi yako. Baada ya kutekeleza kazi yako, andika kwa ufupi (ukurasa mmoja) tathmini ya kazi yako na umkabidhi mkufunzi wako. Mfano wa muhtasari wa Kazi ya Huduma ni kama ifuatavyo: 1. Jina lako 2. Eneo ulilolitumia na hadhira uliyowashirikisha. 3. Muhtasari wa namna muda wako ulivyoenda, namna ulivyojisikia na namna watu walivyoitikia. 4. Ulijifunza nini kupitia mchakato mzima wa kazi yako. Kazi ya huduma inabeba alama 30 ambazo zinawakilisha 10% ya jumla ya maksi zako, hivyo hakikisha unashirikisha yale uliyojifunza kwa ujarisi na ripoti yako iwe yenye kueleweka vizuri.

Utoaji maksi

/ 1 5

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Nafsi ya Roho Mtakatifu

S O M O L A 1

Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kushiriki katika mijadala, na kutendea kazi yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kuelezea uelewa wa msingi wa kikristo kuhusu Mungu kama Utatu. • Kutumia Maandiko kutetea ukweli kwamba Roho Mtakatifu ni Mungu kamili. • Kutumia Maandiko kutetea ukweli kwamba Roho Mtakatifu ni Nafsi ya Kiungu. • Kuelezea neno filioque na kwa ufupi kuelezea kutokukubaliana kwa kitheolojia ambako kumetokea kutokana na neno hilo. • Kuelewa na kutetea sababu za kitheolojia zinazopelekea kuamini kwamba Roho Mtakatifu ametoka kwa Baba na kwa Mwana. • Kuelezea ufafanuzi wa Agostino kuhusu Roho Mtakatifu kama “kifungo cha Upendo” kati ya Baba na Mwana. • Kuelezea kwa nini Roho Mtakatifu lazima aabudiwe na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana. • Kuelezea kwanini somo la kitheolojia la Roho Mtakatifu linaitwa Neumatologia. • Kutoa muhtasari wa mtazamo wa Agano la Kale kuhusu Roho wa Mungu. • Kutumia Maandiko kuelezea kazi ya Roho Mtakatifu ya kutoa uzima katika kuumba na kuuhifadhi ulimwengu. • Kutambua alama kuu zinazohusiana na Roho Mtakatifu katika Maandiko na kuonyesha ni kwa namna gani zinachangia katika uelewa wetu juu ya Roho kama mpaji wa uzima. • Kuelezea ni kwa namna gani majina na vyeo vya Roho Mtakatifu vinatusaidia kumwelewa kama mpaji wa uzima. • Kuelezea kwanini huduma ya Roho ni chanzo cha tumaini.

Malengo ya somo

1

1 6 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Roho Anayemfanya Mungu Ajulikane

Ibada

Soma 1 Wakorintho 2:10-11 na Warumi 8:26. Roho wa Mungu ni wa ajabu sana. Kwa upande mmoja, anafunua mafumbo ya ndani kabisa ya nia na mapenzi ya Baba. Ana maarifa na ufahamu usio na kikomo. Na bado, kwa upande mwingine, anayo huduma maalum ya kuwa karibu nasi, ili kutusaidia kuelewa Mungu ni nani na ni kitu gani anatamani kwetu. Roho Mtakatifu, kwa mujibu wa mafundisho ya 1 Wakorintho 2, ndiye anayetufunulia hekima na siri za Mungu zilizofichika. Na, kama vile somo la Warumi linavyoonyesha, Roho huomba mapenzi ya Mungu ndani yetu na kupitia sisi wakati ambapo fahamu zetu za kibinadamu zimefikia kikomo na hatujui nini au jinsi gani tunapaswa kuomba. Tunapoanza somo letu la theolojia ya Roho Mtakatifu, tunakumbana na kweli kuu kwamba hatuwezi kumwelewa Roho wa Mungu pasipo msaada wa Roho wa Mungu. Ikiwa kwa kweli tutaufahamu ukweli huu, utaweza kuzalisha unyenyekevu na shukrani ndani yetu. Tunanyenyekezwa kwa sababu tunatambua kwamba hatuwezi kumjua Mungu kwa juhudi zetu wenyewe (haijalishi tunajifunza kwa bidii kiasi gani), bali kwa kazi ya Roho pekee. Tunashukuru kwa sababu tunajua kwamba tumempokea Roho kupitia ahadi za kweli za Mungu na kwamba tayari yuko kazini ndani yetu na kati yetu ili kutuongoza kwenye kweli yote. Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (iliyo katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Eh! Baba mwenye neema na mtakatifu, utupe hekima ya kukufahamu, akili ya kukuelewa, bidii ya kukutafuta, subira ya kukungojea, macho ya kukutazama, moyo wa kukutafakari, na maisha ya kukutangaza kwa uweza wa Roho wa Yesu Kristo Bwana wetu. Amina. ~ St. Benedict. From William Lane, S. J. Praying with the Saints . Dublin, Ireland: Veritas, 1989. uk. 26.

1

Kanuni ya Imani ya Nikea na Sala

Hakuna jaribio katika somo hili.

Jaribio

Hakuna Maandiko ya kukariri katika somo hili.

Uhakiki wa Kukariri Maandiko

Hakuna kazi katika somo hili.

Kazi za kukusanya

/ 1 7

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

MIFANO YA REJEA

Theolojia ya Kitabu cha Picha

Chora picha ambayo inamuwakilisha Roho Mtakatifu. Ukishamaliza, ujiandae kuelezea mchoro wako kwa wengine.

1

Kuishindania Imani

Kanisa katika kila kipindi limekuwa likikumbana na “walimu wa uongo” ambao wanayapindisha Maandiko, wakiyatumia kufundisha mafundisho ambayo ni tofauti kabisa na yale ya Yesu na Mitume wake. Mafundisho haya ya uongo (uzushi) yanaonekana “kujizalisha upya,” na kwa sababu hiyo mawazo yaleyale yaliyokosewa yanapata mawakili wapya katika kila kizazi. Wazo moja lisilosahihi kuhusu Roho Mtakatifu ambalo linajitokeza mara kwa mara ni imani kwamba Roho Mtakatifu ni aina fulani ya nguvu ya kiroho (au ufahamu fulani wa kiroho) lakini sio Nafsi ya Kiungu inayoongea na kutenda kama Mungu Aliye Hai. (Katika nyakati zetu, makundi kama Mashahidi wa Jehova na The Unity School of Christianity yanafundisha mtazamo huu wa uongo). Mafundisho ya kikristo maarufu zaidi katika nyakati za sasa yanalenga kuelezea kazi za Roho Mtakatifu; kile ambacho anafanya kwenye maisha ya waamini. Unaweza kufikiri sababu yoyote inayoweza kuonyesha kwamba kufundisha Roho Mtakatifu ni nani kuna umuhimu sawa na kufundisha kazi zake?

2

1

Watatu Katika Mmoja

Tuna maanisha nini tunaposema kwamba Mungu ni Utatu? Ni vielelezo vipi umevisikia vikitumika kujaribu kuelezea Utatu? Kuna vipengele gani vinavyoonyesha uthabiti na udhaifu katika kila kielelezo?

3

1 8 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Nafsi ya Roho Mtakatifu Sehemu ya 1

YALIYOMO

Mch. Terry G. Cornett

Katika sehemu hii ya kwanza, tutajikita katika kumthibitisha Roho Mtakatifu kama Bwana, ambaye kama ilivyo kwa Baba na Mwana, ni mshiriki kamili na mwenye hadhi sawa katika Utatu Mtakatifu. Tutajaribu kuelewa uhusiano alionao na Baba na Mwana na njia ambazo Kanisa limejaribu kuelezea fundisho hili gumu. Hatimaye, tutatilia mkazo ulazima wa kumwabudu Mungu kama Utatu, huku tukimpa utukufu Baba na Mwana na Roho Mtakatifu kwa kiwango kile kile pasipo kuwagawanya. Dhumuni letu katika sehemu hii ya kwanza ya Nafsi ya Roho Mtakatifu ni kukuwezesha kufanya yafuatayo: • Kuelezea uelewa wa msingi wa kikristo kuhusu Mungu kama Utatu. • Kutumia Maandiko kutetea ukweli kwamba Roho Mtakatifu ni Mungu kamili. • Kutumia Maandiko kutetea ukweli kwamba Roho Mtakatifu ni Nafsi ya Kiungu. • Kuelezea neno filioque na kwa ufupi kuelezea kutokukubaliana kwa kitheolojia ambako kumetokea kutokana na neno hilo. • Kuelewa na kutetea sababu za kitheolojia zinazopelekea kuamini kwamba Roho Mtakatifu ametoka kwa Baba na kwa Mwana. • Kuelezea ufafanuzi wa Agostino kuhusu Roho Mtakatifu kama “kifungo cha Upendo” kati ya Baba na Mwana. • Kuelezea kwa nini Roho Mtakatifu lazima aabudiwe na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana.

Muhtasari wa Sehemu ya 1

1

/ 1 9

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

I. Utangulizi

Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video

A. Kanuni ya Imani ya Nikea

1. Tazama kiambatisho Na. 1 kupata nakala ya Kanuni ya Imani ya Nikea.

2. Kwanini kutumia Kanuni ya Imani ya Nikea?

1

3. Biblia ni chanzo pekee cha fundisho kwa Kanisa kisicho na makosa. Kanuni ya Imani ya Nikea sio andiko lenye mamlaka yake binafsi lakini ni kwa sababu, kwa umakini mkubwa, kanuni hii inatoa muhtasari wa kile ambacho Biblia inafundisha.

4. “Ile Mitaguso (mabaraza) ya kale ya Nikea, Konstantinopoli, ule wa kwanza wa Efeso, Kalkedonia, na inayofanana na hiyo ambayo lilifanyika ili kurekebisha makosa, tunaitambua na kuiheshimu kama mitaguso mitakatifu katika mambo yote yahusianayo na mafundisho ya Imani, kwa kuwa haina kitu kingine chochote isipokuwa tafsiri safi na ya kwelii ya Maandiko.” (John Calvin, Institutes, IV, ix.8).

B. Fundisho la Utatu

Utatu ni neno la kifupi linalotumika kueleza katika neno moja kile ambacho Maandiko yanafundisha katika vifungu vingi lakini ambavyo vimelichukua Kanisa muda fulani kutafakari na kuviunganisha katika fundisho linaloeleweka na la pekee... ~ Thomas C. Oden

1. Utatu ni neno ambalo linatumiwa na Kanisa kuelezea namna ambavyo Mungu ni Mungu mmoja, anayeishi milele katika Nafsi Tatu.

2. Maandiko yanasisitiza kwamba Mungu ni mmoja, na kwamba hakuna mwingine isipokuwa Mungu mmoja, na bado yanasisitiza kwamba huyu Mungu mmoja anajifunua mwenyewe kama Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu.

2 0 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

3. Theolojia ya Utatu inathibitisha kwamba washirika wa Utatu kimsingi ni wamoja, wanautofauti, na wana hadhi sawa, kwa pamoja wanaunda Mungu mmoja wa kweli na asiyegawanyika, ambaye milele yupo kama Baba, Mwana na Roho Mtakatifu au kama ambavyo Kanuni ya Imani ya Athanasia inasema: Baba ni Mwenyezi, Mwana ni Mwenyezi, Roho Mtakatifu ni Mwenyezi. Hata hivyo hawa si watatu wenyezi; yupo Mwenyezi mmoja tu.

C. Mungu huyu wa Utatu ndiye ambaye tunakutana naye katika Maandiko kupitia:

1

1. Kuwalenga Watatu

a. Isaaya 6:3 – Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu , ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake. [Zingatia pia ms. 8 ambapo Mungu anasema, “Nimtume nani, naye ni nani atakaye enda kwa ajili yetu?”]

Wakati Mungu alipomtokea Ibrahimu kwenye mialoni ya Mamre, alimtokea katika sura ya “watu watatu wamesimama mbele yake” (Mwa. 18:2), na bado mmoja aliyefunuliwa. Katika kutangaza ujio wa uzao wa mtoto kwa bibi kizee Sara, walizungumza kama mmoja. “Ibrahimu aliwaona watatu, akamsujudia mmoja”, anafafanua Ambrose. ~ Thomas C. Oden. The Living God. San Francisco: HarperSanFrancisco, 1987. uk. 191 inaonekana wazi kwanba ni Bwana

b. Ufunuo 4:8 – Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu , Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.

2. Kutokea kwa Watatu

a. Mwanzo 18:2-3,10 - Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi, akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako... . [Bwana] Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.

/ 2 1

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

b. Mathayo 3:16-17 – Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu , ninayependezwa naye.

3. Kanuni ya Ubatizo katika Utatu Mathayo 28:19 – Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.

1

4. Baraka katika Utatu

a. Hesabu 6:24-26 – BWANA akubariki, na kukulinda ; BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani.

b. 1 Petro 1:2 – kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kunyunyiziwa damu ya Yesu Kristo . Neema na amani na ziongezwe kwenu.

c. 2 Wakorintho 13:14 - Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.

II. Roho aliye Bwana: Maandiko yanamuonyesha Roho Mtakatifu kama Mungu kamili. Tuna amini katika Roho Mtakatifu, Bwana na Mpaji wa uzima, ambaye anafanya kazi pamoja na Baba na Mwana, ambaye sambamba na Baba na Mwana anaabudiwa na kutukuzwa, ambaye alizungumza kupitia manabii.

Tazama Ray Pritchard, Names of the Holy Spirit , (Chicago: Moody Press, 1995), ukurasa wa 36, 59, 158, 173, 196, 207.

2 2 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

A. Maandiko yanamtambua Roho Mtakatifu moja kwa moja kama Mungu.

1. Matendo 5:3-4

2. Luka 1:35

3. 2 Petro 1:21

1

4. 2 Wakorintho 3:17-18

B. Roho ana uwezo wa kiungu. 1 wakorintho 2:10-11 – Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. C. Roho ana sifa na tabia za Kiungu. MunguBaba,MunguMwana, na,MunguRohoMtakatifuwanazungumzwa kama Nafsi tofauti katika Maandiko lakini kila mmoja anazungumziwa kama mwenye sifa zilizo sawa na Mungu. (Roho yuko vile Mungu alivyo na anafanya kile ambacho Mungu anafanya). 1. Asili ya Kiungu: Roho ameelezewa kama mwenye sifa ambazo ziko kwa Mungu peke yake: Kujua yote (Isa. 40:13; 1 Kor. 2:10-12), kuwepo kila mahali (Zab. 139:7 10), kuwa na uweza wote (Ayu 33:4; Zab. 104:30; Rum. 15:18, 19), umilele (Ebr. 9:14). ~ Thomas C. Oden. Life in the Spirit: Systematic Theology, Vol 3 .

/ 2 3

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

2. Kazi za Kiungu:

a. Anaifunua kweli ya Mungu (1 Kor. 2:10; Mdo 28:25)

b. Anatoa karama za rohoni (1 Kor. 12)

c. Anatakasa dhambi (2 The. 2:13; 1 Pet. 1:2)

1

d. Anatoa uzima kwa waliokufa (Rum. 8:11)

e. Analiongoza Kanisa (Mdo 13:2; 15:28)

3. Majina ya Kiungu:

a. Roho wa Mungu (Mwa. 41:38; 2 Kor. 3:3; Efe. 4:30)

b. Roho wa Yesu Kristo (Mdo 16:7; Rum. 8:9)

c. Roho wa Bwana (Isa. 61:1; Mik. 2:7)

d. Roho wa Utukufu (1 Pet. 4:14)

e. Roho wa Utakatifu (Rum. 1:4)

f. Mtetezi wa Kristo (1 Tim. 3:16)

2 4 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

D. Roho anazo heshima za Kiungu Mathayo 12:32 – Naye mtu yeyote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.

E. Roho Mtakatifu ni nafsi

1. Maelezo yake kama nafsi

1

a. Yohana 16:13-14

b. Neno linalotafsiriwa kama roho kwa kiyunani ni neno lisilo na jinsia na wazungumzaji wa kiyunani humtaja roho kama “kitu”. Lakini katika Yohana 16:13-14, pale ambapo Yesu anaongea kuhusu Roho Mtakatifu, Yesu hasemi, “lakini itakapokuja hiyo roho ya kweli, itawaongoza iwatie kwenye kweli yote”; badala yake anasema “atawaongoza awatie kwenye kweli yote”.

2. Utambulisho wake kama nafsi: Roho anafanya kazi kama “mwingine aliye kama Yesu,” jambo ambalo lisingewezekana kama asingekuwa nafsi.

a. Yesu aliongelea kuhusu ujio wa Roho kama “msaidizi mwingine ( allon )” * Yohana (14:16). Hii ina maana kwamba Yesu tayari ameshakuwa msaidizi ( paraclete) akiwa pamoja na wanafunzi wake, na kwamba Roho atakuja kuchukua nafasi yake na kuendeleza

* Neno Msaidizi linatokana na neno la Kiyunani parakl  tos ambalo lina maana ya “kuitwa kuwa upande wa mtu fulani.” Neno hilo kwa kawaida lilitumika kama neno la kisheria likiwa na maana ya wakili, mtu ambaye alisaidia katika utetezi wa kesi mahakamani kwa niaba ya mtu mwingine. Kwa ujumla zaidi, linaweza kumaanisha mtu yeyote ambaye anabeba jambo la mtu mwingine au mtu anayemwombea mtu mwingine (kama Bwana Yesu katika 1 Yohana 2:1). Ndilo neno ambalo Yesu alilitumia kwa habari ya Roho Mtakatifu katika Yohana 14:16; 14:26; 15:26 na 16:7. Limetafsiriwa mara kadhaa kwa namna tofauti-tofauti kwa kiingereza na hatimaye kwa kiswahili kama neno Msaidizi, Mfariji, Wakili, Mshauri, na Rafiki.

/ 2 5

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

huduma yake na wanafunzi. (George Eldon Ladd, A Theology of the New Testament, uk. 294).

b. Yohana 14:16-18 – Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. 18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. (Linganisha na Yohana 16:7).

1

c. Katika Yohana 16:7-15, Yesu anaahidi kwamba atakapokuja Roho Mtakatifu atafanya kwa wanafunzi kila kitu ambacho yeye Yesu alikifanya alipokuwa pamoja nao katika mwili.

3. Roho anatenda kazi ambazo zinaweza tu kutendwa na nafsi.

a. Roho anatenda kazi za mshauri/wakili ambazo zinaonyesha kazi za kiutu na za kimahusiano, yaani, kazi za kufariji, kutia moyo, na kusaidia (tazama Yohana 16).

b. Roho anafundisha. (1) Luka 12:12

(2) Yohana 14:26 (3) Yohana 16:8 (4) 1 Wakorintho 2:10

c. Roho ana mapenzi yake binafsi, anaelekeza, na kuongoza. (1) 1 Wakorintho 12:11

(2) Matendo 8:29 (3) Matendo 13:2 (4) Matendo 16:7

2 6 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

(5) Warumi 8:14

d. Roho anashuhudia. (1) Yohana 15:26 (2) 1 Yohana 5:6.

e. Roho anawaombea Wakristo Rum 8:26 (linganisha na Yuda 1:20).

1

4. Roho katika Maandiko ameitikiwa kama nafsi.

Kuna vifungu kadhaa vya Maandiko pia ambavyo vinamtofautisha Roho Mtakatifu na nguvu zake. Luka 1:35; 4:14; Mdo 10:38; Rum. 15:13; 1 Kor. 2.4. Vifungu vya Maandiko vya namna hii vingekuwa vinaonyesha kitu kilekile tu ambacho kimejirudia mara mbili, vingekuwa havina maana na upuuzi, kama vingetafsiriwa katika dhana ya kwamba Roho Mtakatifu ni kani (nguvu) tu. Hili linaweza kuonyeshwa kwa kubadilisha Jina “Roho Mtakatifu” na neno kama “nguvu” au “ushawishi.” ~ L. Berkhof. Systematic Theology . Grand Rapids, MI: Eerdmans, 1941. uk. 96.

a. Anaweza kuhuzunishwa na kufanyiwa jeuri. (1) Isaya 63:10 (2) Waefeso 4:30 (3) Waebrania 10:29

b. Watu wanaweza kujaribu kumdanganya, Mdo 5:3.

5. Nafsi ya Roho ni tofauti na nguvu zake.

a. Matendo 10:38 -... habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huku na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.

b. 1Wakorintho 2:4 -... Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima, yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu.

/ 2 7

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

III. Roho Atokaye kwa Baba na kwa Mwana.

A. Fundisho la Filioque Kuna neno dogo katika Kanuni ya Imani ambalo halikuwa katika maandishi ya awali ambayo yalikubaliwa na Mtaguso wa Kanisa wa mwaka 381. Neno hilo dogo linaloitwa filioque [fee-lee-OH-kway], ambalo ni neno la kiyunani linalomaanisha “na Mwana,” limekuwa chanzo cha mjadala mkubwa katika Kanisa. Sehemu ya Mashariki ya Kanisa ambayo baadaye ilikuja kuwa kanisa la Kiothodoksi la Mashariki bado inatumia muundo ule wa awali wa Kanuni ya Imani. Sehemu ya Magharibi ya Kanisa, ambayo baadaye ilikuja kuwa Kanisa Katoliki la Rumi, ilikuwa inaendelea kupambana na uzushi uliokuwa ukiendelea kupinga Uungu kamili wa Yesu Kristo. Ili kulipa mizizi fundisho la Utatu, neno “na Mwana” liliongezwa ili kufanya ieleweke zaidi kwamba Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu daima wameunganika pamoja katika utendaji wao na asili yao. 1. Kanisa la Mashariki lilipinga kwa kusema kwamba Mungu Baba pekee ndiye chanzo cha vitu vyote. (Japokuwa Nafsi zote tatu za Utatu ni za milele na ziko sawa, bado ni kweli kwamba Mwana alitolewa na Baba na sio Baba kutolewa na Mwana). Kwa sababu hiyo Maandiko yanasema hivi: Yohana 15:26 – Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.

1

2. Kanisa laMagharibi laKatoliki na (baadaye)makanisa yaKiprotestanti ambayo yalijitenga nalo yalifanya makubaliano haya kama utetezi wao dhidi ya makanisa ya Kiothodoksi ya Mashariki.

a. Roho Mtakatifu, haitwi tu “Roho wa Mungu” bali pia “Roho wa Yesu”.

(1) Yohana 14:16-18 (2) Yohana 16:13-14 (3) Wagalatia 4:6

2 8 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

(4) Wafilipi 1:19 (5) Warumi 8:9.

b. Roho Mtakatifu sio wa Baba peke yake, au Roho wa Mwana peke yake, bali ni Roho wa Baba na wa Mwana. Kwa maana imeandikwa, “Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu. (Mathayo 10:20)”; na tena imeandikwa: “Mtu yeyote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake (Rum. 8:9).” Pale ambapo Baba na Mwana wanatajwa kwa namna hii, Roho Mtakatifu anaeleweka, Yule ambaye Mwana mwenyewe anamzungumzia katika Injili, kama Roho “atokaye kwa Baba” (Yohana 15:26), na kwamba “Atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha” (Yohana 16:14) (Mt. Damascus wa I, 382 B.K.). c. Kusudi na kazi za Roho vinatokana na Baba na Mwana kwa pamoja. Yeye ni karama ambayo imetolewa kwetu na Baba na Mwana kwa pamoja. (1) Yesu anawabatiza waamini kwa Roho Mtakatifu, Luka 3:16. (2) Yesu anamimina Roho Mtakatifu aliyeahidiwa na Baba, Mdo 2:33. (3) Yesu anawaalika wale walio na kiu ya Roho kwenda kwake na kunywa, Yohana 7:37-39. (4) Yesu “alimpulizia” Roho Mtakatifu kwa wanafunzi wake, Yohana 20:21-22. d. Kila nafsi katika Utatu inapaswa kutofautishwa na nyingine kitheolojia. (Baba sio Mwana sio Roho). (1) Baba hatokani na yeyote, hajafanywa wala kuumbwa, wala kuzaliwa. (2) Mwana ni wa Baba peke yake, hajafanywa, wala hajaumbwa lakini amezaliwa.

1

/ 2 9

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

(3) Roho ni wa Baba na wa Mwana, hajafanywa, hajaumbwa wala hajazaliwa, bali ametolewa (sehemu ya Kanuni ya Imani yaa Athanasia ).

Muungano kati ya Baba na Mwana ni kitu kilicho thabiti sana kiasi kwamba muungano huu wenyewe tu pia ni Nafsi. Najua hili ni gumu sana kueleweka kwa akili ya kibinadamu, lakini litazame hivi. Unajua kwamba miongoni mwa wanadamu, pale wanapokutana pamoja kama familia, au chama au muungano wa kibiashara, watu huzungumza kuhusiana na “roho” ya familia kuhusiana na “roho” ya miungano hiyo kwa sababu wanachama mmoja mmoja wanapokuwa pamoja huzalisha njia fulani za kuzungumza na kuenenda ambazo wasingekuwa nazo kama wangekuwa kila mmoja mahali pake. Ni kama aina fulani ya nafsi ya jumuiya inazaliwa. Bila shaka, sio nafsi halisi: ni kwamba tu inakuwa kama nafsi. Lakini hiyo ni moja tu kati ya zile tofauti zilizopo kati ya Mungu na sisi. Kile kinachotokea katika muungano wa Baba na Mwana ni Nafsi halisi, na kusema kweli ni ya tatu kati ya zile Nafsi tatu ambazo ni Mungu. ~ C. S. Lewis. Mere hiyo, au ya chama au ya muungano wa kibiashara. Wanazungumza

B. “Kifungo cha Upendo”

1. Mt. Agostino, katika kutafakari juu ya tofauti hii ya kitheolojia iliyopo kati ya washirika wa Utatu, alitoa maelezo haya muhimu kwa habari ya Roho Mtakatifu. Alimwita “Kifungo cha Upendo” kati ya Baba na Mwana.

1

2. Roho anatambulishwa kwa ukaribu sana katika Maandiko pamoja na Upendo wa Mungu.

a. Upendo wa Mungu umemiminwa katika mioyo yetu kupitia Roho Mtakatifu, Rum. 5:5.

b. Mungu ni upendo, 1 Yohana 4:8.

c. Mungu ni Roho, Yohana 4:24.

d. Tukipendana,Munguhukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu... kwa kuwa ametushirikisha Roho wake, 1 Yohana 4:12-13.

3. Roho wa Mungu ni upendo unaotoka kwa Baba na Mwana. “Kipawa hiki cha Upendo” au “Kifungu cha Upendo” ni sehemu yenye utashi ya Uungu.

Christianity . New York: Macmillian, 1952. uk. 152.

3 0 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

4. Hivyo Agostino, anaelezea uhusiano wa Utatu kwa namna hii:

a. “Yeye anayempenda ambaye ametoka kwa Yeye mwenyewe” (kwa maneno mengine, Baba ndiye anayempenda Mwana ambaye alimtoa). (Tazama Luka 20:13; Yohana 5:20; Kol. 1:13; Efe. 1:6; 2 Pet. 1:17.)

b. “Yeye anayempenda Yule ambaye kwa yeye, yupo” (kwa maneno mengine, Mwana ndiye anaye mpenda Baba ambaye alitoka kwake). (Tazama Yohana 5:19; Yohana14:31; Yohana 17:1).

1

c. “Na Upendo wenyewe” (kwa maneno mengine, Roho Mtakatifu ndiye Kifungo cha Milele cha Upendo kati ya Baba kwa Mwana (tazama, Marko 1:10-11; Marko 9:7; Yohana 3:34-35; Gal. 4:6).

5. Kazi ya kipekee ya Roho Mtakatifu katika Utatu ni kuwa kifungo cha ushirika wa Upendo kati ya Baba na Mwana.

a. Yohana 16:13-15

b. 2 Wakorintho 13:14

c. Waefeso 4:3

/ 3 1

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Kwa namna ya ajabu sana Roho anaweza kuelezwa kuwa anawaunganisha Baba na Mwana katika upendo na kutolewa kama upendo kati yao.... Upendo huunganisha watu wanaothaminiana, na kwa upande wa Mungu upendo unafikia ukamilifu katika Nafsi ya tatu, ambaye anapendwa na Baba na Mwana. Nafsi ya tatu, Asiye na jina maalum kama “Baba” au “Mwana” anatosheka na jina la jumla la Mungu la “roho.” Inatosha kwake kujulikana kuwa “kifungo cha upendo”…. Anafurahia uhusiano wa upendo wa dansi ya kimungu na kushangilia katika upendo usio na ubinafsi unaowaunganisha Baba na Mwana. Anafurahia kuingiza viumbe kwenye muungano na Mungu, ngoma ya Utatu na mchezo wa sabato wa uumbaji mpya. ~ Clark Pinnock. Flame of Love . Kurasa za 38-39.

1

IV. Yeye ambaye Pamoja na Baba naMwana Anaabudiwa na Kutukuzwa.

A. Mantiki ya Utatu: Hitimisho thabiti la mjadala wote hapo juu ni kwamba Roho Mtakatifu anastahili kupewa heshima kama Mungu.

1. Maandiko yanaonyesha umoja usiovunjika na usawa kati ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, kile anachostahili mshirika mmoja wa Utatu, wanastahili washirika wengine wote.

Nyaraka za mitume kwa makanisa (kama vitabu vya Injili vyenyewe) zilimuonyesha Mungu kama Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, na kujenga msingi imara sana katika kuongelea kuhusu Mungu katika lugha ya Utatu (mfano. 2 Kor. 13:13; Efe. 2:18; 1 Pet. 1:2; Yuda 20-21). Kanisa la kwanza liliazima na kuakisi lugha hii lilipokuwa linaomba na kuabudu.

2. Isaya 6:1-3 (Linganisha na Ufu. 4:8)

3. “[Katika Isaya 6] Maserafi wanatamka sifa, kundi lote la waliobarikiwa linatamka sifa, kwa vile wanavyomwita Mungu Mtakatifu, Mwana Mtakatifu na Roho Mtakatifu.” (Ambrose, Of the Holy Spirit, Bk. III, NPNF, ms. 10, uk. 151).

B. Roho anaabudiwa katika Kanisa kwa Kanuni za Imani za ki-Utatu, maombi ya ki-Utatu, nyimbo za tenzi za ki-Utatu, na matamko ya Baraka ya ki-Utatu.

3 2 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

1. Kutamka Kanuni ya Imani ya Nikea na/au ya Mitume wakati wa ibada.

2. Maombi yenye miisho kama: “tunaomba haya kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu, anayeishi na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja, sasa na hata milele, Amina.”

3. Nyimbo /tenzi za rohoni za Utatu (Mfano. Doksolojia, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Uje Ee Mfalme Mwenyezi, Gloria Patri)

1

4. Baraka za utatu kama: “Baraka za Mungu Mwenyezi, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, ziwe kati yenu sasa, na zikae nanyi siku zote. Amina” au “Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote” (2 Kor. 13:14).

Hitimisho

Roho Mtakatifu ni Nafsi ya tatu ya Mungu mmoja wa Utatu. Yeye ni Nafsi inayotofautishwa na nafsi nyingine katika Uungu na inayofikiri, kutenda, na kupenda kikamilifu kama Baba na Mwana na ambaye anashiriki kikamilifu Asili yao ya Uungu. Wakati fulani Kanisa limetofautiana kuhusu jinsi ya kufafanua asili halisi ya mahusiano kati ya washirika wa Utatu (mf . Yale matumizi ya neno filioque ) lakini wote wanakubaliana juu ya uungu kamili, utu au nafsi, na usawa wa kila mshirika. Kwa Wakatoliki na Waprotestanti, maelezo ya Mtakatifu Agostino kuhusu Roho Mtakatifu kama “kifungo cha upendo” kati ya Baba na Mwana yamethibitika kuwa mlinganisho muhimu na wa kudumu. Kwa kuzingatia ushahidi wa Maandiko, Kanisa daima limemwabudu Mungu kama Utatu likitoa utukufu kwa Baba na kwa Mwana na kwa Roho Mtakatifu kwa usawa na bila kuwagawanya.

/ 3 3

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Tafadhali chukua muda wa kutosha uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yametokana na video. Tumekuwa tukifanyia kazi mawazo magumu sana kuhusu asili ya Mungu na uhusiano kati ya Baba, Mwana, na Roho. Ingawa mawazo haya yana changamoto, ni ya muhimu kwa sababu ufahamu wetu juu ya Mungu utaathiri kila sehemu ya imani na maisha yetu. Maswali yafuatayo yamekusudiwa kutusaidia kupitia na kuelewa kikamilifu zaidi yale ambayo tumejifunza. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko kujenga hoja zako! 1. Kwa nini ufahamu wa Utatu ni msingi wa ufahamu sahihi wa Roho Mtakatifu? 2. Je, tuna ushahidi gani kwamba Roho ni Mungu kamili? 3. Je, tuna uthibitisho gani kwamba Roho ni Nafsi ya Kiungu? 4. Kwa nini Waprotestanti na Wakatoliki wanaamini kwamba Roho “ametoka kwa Baba na Mwana”? 5. Ni njia zipi ambazo Baba, Mwana, na Roho wanaweza kutofautishwa baina yao? (kwa namna gani wanatofautiana?) 6. Ni kwa msingi gani wa kibiblia ambapo Kanuni ya Imani ya Nikea inasisitiza kwamba Roho anapaswa “kuabudiwa na kutukuzwa”?

Sehemu ya 1

Maswali kwa wanafunzi na majibu

1

Nafsi ya Roho Mtakatifu Sehemu ya 2: Mpaji wa Uzima

Mch. Terry G. Cornett

Hii ni sehemu ya pili ya somo la kwanza la moduli hii, lenye kichwa cha Nafsi ya Roho Mtakatifu . Katika sehemu hii tutaangalia kwa makini mada kuu inayounganisha kazi nyingi za Roho Mtakatifu ulimwenguni. Tutaona kwamba Roho ndiye atoaye uhai kwa ulimwengu kupitia kazi yake katika uumbaji na upaji. Tutachunguza baadhi ya alama za kawaida, majina, na vyeo vinavyotumiwa kumwelezea Roho Mtakatifu katika Maandiko na kuchunguza jinsi kila moja ya alama, majina na vyeo hivyo inavyochangia katika ufahamu wetu juu ya Roho kama Mpaji wa Uhai. Hatimaye, tutahitimisha kwa mjadala wa jinsi huduma ya upaji uzima ya Roho inavyoleta tumaini la siku zijazo.

Muhtasari wa Sehemu ya 2

3 4 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Malengo yetu kwa sehemu hii, Mpaji wa Uzima , nikukuwezesha: • Kuelezea kwanini somo la kitheolojia la Roho Mtakatifu linaitwa Neumatologia. • Kutoa muhtasari wa mtazamo wa Agano la Kale kuhusu Roho wa Mungu. • Kutumia Maandiko kuelezea kazi ya Roho Mtakatifu ya kutoa uzima katika kuumba na kuuhifadhi ulimwengu. • Kutambua alama kuu zinazohusiana na Roho Mtakatifu katika Maandiko na kuonyesha ni kwa namna gani zinachangia katika uelewa wetu juu ya Roho kama mpaji wa uzima. • Kuelezea ni kwa namna gani majina na vyeo vya Roho Mtakatifu vinatusaidia kumwelewa kama mpaji wa uzima. • Kuelezea kwanini huduma ya Roho ni chanzo cha tumaini.

1

I. Mpaji wa Uzima

Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video

Tunamwamini Roho Mtakatifu, Bwana na Mpaji wa Uzima , atokaye kwa Baba na kwa Mwana, ambaye pamoja na Baba na Mwana anaabudiwa na kutukuzwa, ambaye alinena na manabii.

II. Pumzi ya Mungu yenye Nguvu

A. Somo kuhusu fundisho la Roho Mtakatifu linajulikana kama Neumatologia (Pneumatology).

1. Pneuma ni neno la Kiyunani lenye maana ya “upepo au pumzi au roho.”

2. Neno la kiebrania ruach (ambalo linatumika katika Maandiko ya Agano la Kale) linabeba maana ileile ya msingi ya “upepo au pumzi au roho.”

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker