Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
1 0 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Matokeo ya mwisho wa kozi yatatolewa katika mfumo wa gredi kwa kutumia skeli ya kutunuku matokeo kwa mtindo wa herufi zenye alama chanya na hasi, kisha alama za gedi yako ya ufaulu katika kazi mbali mbali zitajumlishwa na kugawanywa kwa idadi ya kazi na vipimo vingine husika ili kupata wastani wa matokeo yako ya mwisho. Kuchelewesha au kushindwa kabisa kukabidhi kazi zako kutaweza kuathiri matokeo yako. Hivyo, ni vyema kupangilia shughuli na muda wako mapema na kuwasiliana na mkufunzi wako endapo kutakuwa na changamoto yoyote. Kama sehemu ya ushiriki wako katika kusoma moduli ya Mungu Roho Mtakatifu , utahitajika kufanya kazi ya ufafanuzi wa Maandiko (uchunguzi wa ndani ya Maandiko yenyewe) kwa kutumia andiko mojawapo kati ya Maandiko yafuatayo kuhusiana na kazi ya Roho Mtakatifu: Yohana 14:15-18 Warumi 8:1-27 1 Wakorintho 2:9-16 Yohana 16:7-11 Warumi 8.12-17 Wagalatia 4:4-7 Dhumuni la kazi hii ni kukupa fursa ya kufanya utafiti wa kina wa kifungu kinacholengwa zaidi cha Maandiko kuhusiana na kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa kutumia kifungu hicho kama msingi, fikiria kwa makini kuhusu njia ambazo Maandiko haya yanaweka wazi kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha ya mwamini, kanisa, na ulimwengu. Unaposoma sehemu hiyo, tumaini letu ni kwamba uchambuzi wako utaongeza ufahamu wako wa namna ambavyo Roho Mtakatifu anafanya kazi ili kukamilisha kusudi la Mungu Ulimwenguni. Vilevile tuna shauku kwamba Roho akupe ufahamu kuhusiana na namna ya kuhusianisha maana yake na safari yako binafsi kama mwanafunzi, pamoja na kazi ya uongozi ambayo Mungu amekupa katika kanisa na huduma yako. Hii ni kazi ya kujifunza Biblia, na ili kufanya kazi ya ufafanuzi, ni lazima udhamirie kuelewa maana ya andiko husika katika muktadha wake. Ukishajua andiko lilimaanisha nini kwa wasomaji wake wa kwanza, unaweza kupata kanuni zinazotuhusu sisi sote leo, na kuzihusianisha kanuni hizo na maisha. Mchakato wa hatua tatu rahisi unaweza kukuongoza katika jitihada zako binafsi za kujifunza kifungu cha Biblia: 1. Je, Mungu alikuwa akisema nini kwa watu katika muktadha wa asili wa andiko husika? 2. Ni kanuni gani ambazo andiko hili linafundisha ambazo ni kweli kwa watu wote kila mahali, ikiwa ni pamoja na sisi leo ? Kazi za ufafanuzi wa Maandiko
Dhumuni
Mpangilio na muundo
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker