Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

1 0 0 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

3. Kuna Maandiko ambayo yanaweza kutajwa kuunga mkono Mitazamo yote miwili, ule wa hatua moja na wa hatua nyingi.

a. Nyaraka za Paulo zinaelekea kusisitiza kwa nguvu zaidi ujio wa Roho Mtakatifu wakati wa mtu kuokoka na kazi yake ya kutuunganisha na Kristo kama tendo kuu la Ubatizo wa Roho Mtakatifu.

b. Vitabu vilivyoandikwa na Luka (Kitabu cha Luka na Matendo ya Mitume) vinaelekea kusisitiza kwa nguvu zaidi kazi ya Roho Mtakatifu katika kuja juu ya mtu ili kumwezesha kuhudumu kwa nguvu (kushuhudia) kama tendo muhimu la ubatizo wa Roho. Nguvu hii ya miujiza mara nyingi inaonekana kuzungumzwa kama hatua ya pili ya kazi ya Roho. c. Paulo na Luka hawapingani bali wanakazia pande zinazotofautiana za kweli moja. Iwe tunashikilia mtazamo wa hatua moja au mtazamo wa hatua nyingi, ni muhimu kwamba tuwachukulie Paulo na Luka, wote wawili, kwa uzito na kujitahidi kuelewa jinsi maoni yao yanavyofanya kazi pamoja ili kueleza kweli moja kuhusu Roho Mtakatifu.

3

B. Mtazamo wa Ubatizo wa Roho kama Tendo la Mara Moja Tu

1. Mtazamo wa ubatizo wa Roho kama tendo la mara moja tu mara nyingi huitwa mtazamo wa Makanisa ya Reformed . Ufahamu huu wa ubatizo wa Roho ndio utaupata kirahisi katika makanisa yenye asili ya Ki-Protestanti, makasina ya Reformed, au ya Ki-Baptisti, pamoja na mengine kadhaa.

2. Kuunganishwa na Kristo ndio ufunguo wa kuuelewa wokovu Kuunganishwa na Kristo katika uzima, mauti, na kufufuka kwake ndiko kuna mtofautisha mkristo na asiye mkristo. Kwa sababu ya

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker