Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 1 0 5
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
utakaso kamili unaweza tu kupokelewa kutoka kwa Roho Mtakatifu na kazi yake ndani ya mwamini (taz. kiambatisho cha 22 kwa ufafanuzi zaidi wa “utakaso kamili” katika makanisa haya ikiwa ni pamoja na ushahidi wa Maandiko na namna dhana hii inavyohusiana na ubatizo katika Roho Mtakatifu). (4) Utakaso ni tendo tofauti na kuzaliwa upya na ni lazima ufuate baada tu ya wokovu. Ingawa huu unaweza kutokea mara moja, lakini mara nyingi huchukua miaka kadhaa kabla ya kutokea kwake. (5) Ubatizo katika Roho Mtakatifu ni tukio la pili baada ya kuongoka ambapo Roho Mtakatifu humleta mtu katika “ukamilifu wa Kikristo” au “utakaso kamili.” Ni njia inayompa mtu nia, shauku na uwezesho wa kuishi maisha matakatifu. Hilo lamaanisha kujiepusha na dhambi za makusudi na kutembea katika upendo kwa Mungu na watu wengine. Ni tendo kubwa la tofauti ambapoMkristo anapata “kukamilishwa katika upendo” na kuwezeshwa kuishi maisha matakatifu. Hii mara nyingi huitwa “baraka ya pili” au “kazi ya pili ya neema.” (b) “Ubatizo wa Roho Mtakatifu” unapokelewa wakati gani? Inatofautiana kwa kila mtu, lakini kwa kawaida ni baada ya kuhesabiwa haki (kuongoka). (c) “Ubatizo wa Roho” unapokelewaje? Kwa njia ya toba na imani, na kutafuta kwa bidii katika maombi. (d) Je, ni ushahidi au uthibitisho gani unaoonyesha kwamba “ubatizo wa Roho” umetokea? Utakatifu wa maisha, unaofafanuliwa kama ushindi juu ya dhambi zinazojulikana na upendo kwa wengine. (6) Muhtasari wa msimamo wa makanisa ya Holiness (a) “Ubatizo katika Roho Mtakatifu” ni nini?
Utakaso kamili ni kazi ya pili ya uhakika ya neema inayotendwa na ubatizo wa Roho Mtakatifu ndani ya moyo wa mwamini baada ya kuzaliwa upya, inayopokelewa mara moja kwa imani, ambapo moyo huoshwa na uharibifu wote na kujazwa na upendo kamili wa Mungu. ~ A. M. Hills, iliyonukuliwa katika J. Kenneth Grider. Wesleyan Holiness Theology . uk. 439.
3
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker