Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
1 0 6 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
b. Ubatizo katika Roho Mtakatifu: Mtazamo wa Kipentekoste (1) Chimbuko katika Maandiko: kutumia Kitabu cha Matendo ya Mitume kama chanzo cha msingi cha kuelewa ubatizo katika Roho Mtakatifu (ona “What can the Bible Stories Teach Us?” cha Keener,kiambatisho, Roho Mtakatifu: Kipawa na Mpaji kwa maelezo na utetezi wa mtazamo huu). Wapentekoste kihistoria walitegemea simulizi za Luka kuwekamsingi wa theolojia yao na wakatoa hoja kwamba kauli za Paulo katika Nyaraka (ambazo kwa ujumla zinaelekezwa katika kutatua matatizo mahususi ya Kanisa), lazima zitafsiriwe kwa kuzingatia mtazamo mpana zaidi wa vitabu vya Injili na Matendo ya Mitume. (2) Wapentekoste wanaamini kwamba kuna tofauti kati ya Roho kukaa ndani ya mwamini na tendo la kujazwa. Wapentekoste mara nyingi hufundisha kwamba Roho hukaa ndani ya Mkristo pale tu anapookoka, lakini huwajaza wakati wa ubatizo wa Roho. (3) Baadhi ya Wapentekoste hufundisha kwamba tunapookoka, “Roho Mtakatifu hutubatiza katika Kristo” ( 1 Kor. 12:13 ), lakini ubatizo katika Roho ni tendo tofauti la wakati tofauti ambapo “Kristo hutubatiza katika Roho Mtakatifu” ( Marko 1:8 ). Hivyo, ubatizo katika RohoMtakatifu ni tukio linalotokea baada ya kuoka na huleta nguvu kwa ajili ya utume na huduma (ling. Mdo 1:4, 8; 8:14-16). (4) Kwa Wapentekoste wengi, uthibitisho wa kwanza (na wa lazima) wa kubatizwa kwa Roho Mtakatifu ni kunena kwa lugha, kulingana na mtindo wanaouona katika Kitabu cha Matendo (Mdo 2:1-4; 10:45-46; 19:5-6), tazama pia Marko 16:17-18). (5) Muhtasari wa msimamo wa Kipentekoste (a) “Ubatizo katika Roho Mtakatifu” ni nini?
3
Ni tukio mahususi na tofauti ambapo mkristo anapokea ujazo wa nguvu za Roho Mtakatifu ili kuhusika kikamilifu katika huduma na utume.
(b) “Ubatizo wa Roho Mtakatifu” unapokelewa lini?
Inatofautiana kwa kila mtu lakini kwa kawaida ni baada ya kuhesabiwa haki (kupokea wokovu).
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker