Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

/ 1 1 9

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Kama hili ni kweli, ni muhimu sana kwamba makanisa yatambue na yatumie vyema karama za rohoni za washirika wao. Kwa kuzingatia uzoefu wako, tunawezaje kuwasaidia watu katika makusanyiko yetu kugundua na kutumia karama ambazo Roho amewapa?

Zoezi la Kujazia Sentensi: Roho Anayekaa Ndani Yetu

Ninafahamu zaidi kwamba Roho Mtakatifu anaishi ndani yangu pale ambapo ___. Baada ya kumaliza jibu lako, mgeukie jirani na chukua dakika chache kumshirikisha ulichojibu na kusikiliza vile alivyojibu pia.

2

Kuimba kuhusu Utakaso

Nyimbo na tenzi ni njia zenye ufanisi za kufundisha na kujifunza kweli za Biblia. Baadaye, tutakuwa tunazungumza juu ya kazi ya Roho katika kututakasa (kututenga kwa ajili ya kutumiwa na Mungu). Hii ina maanisha kwamba Roho anatufanya sisi kuwa watakatifu (yaani kuwa kama Kristo) ili kwamba maneno, matendo, na mitazamo yetu iakisi kweli na tabia ya Mungu. Ni nyimbo au tenzi gani ambazo mnaziimba katika kanisa ambazo zinazungumza kuhusu nia ya Mungu kwamba tuwe watakatifu au kazi yake katika kutufanya watakatifu?

3

4

Uwepo Wenye Nguvu wa Roho Mtakatifu (Sehemu ya Pili) Sehemu ya 1: Roho Anayetoa Karama na Kukaa Ndani Yetu

YALIYOMO

Mch. Terry G. Cornett

Malengo yetu katika sehemu hii, Roho Anayetoa Karama na Kukaa Ndani Yetu, ni kukuwezesha kufanya yafuatayo: • Kuelewa ufafanuzi wa karama za rohoni na uweze kueleza makusudi yake. • Kutambua, kufafanua, na kuainisha karama za rohoni ambazo zimeelezewa katika Agano Jipya. • Kutambua na kuelezea kanuni za msingi za kitheolojia zinazohusiana na karama za rohoni. • Kuelezea maana na umuhimu wa Roho kukaa ndani ya waamini.

Muhtasari wa Sehemu ya 1

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker