Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 1 2 7
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
(2) Nini kinakuletea utoshelevu wa kimungu? Waefeso 2:10 inasema, “Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.” Tunapo yafanya yale ambayo tuliumbwa kuyafanya, tunapata hisia za utoshelevu na hali ya kutimizwa kwa kusudi. Hii haimanishi kwamba kuhudumu katika karama zetu hakuhusishi kujidhabihu, jitihada, na hata kufadhaika. Inamaanisha kwamba ndani kabisa katika vilindi vya mioyo yetu tunajua kwamba tunatimiza kusudi letu tulilopewa na Mungu na kwamba tunachukua nafasi yetu katika kulisaidia Kanisa kutimiza utume ambao Mungu ameliitia. (3) Roho Mtakatifu anashuhudia nini ndani yako? Roho ni sauti ya Mungu iliyo hai inayozungumza. Ikiwa Roho ndiye anayetoa karama, basi yeye pia ndiye anayetuongoza ili kuzitambua kwa ufasaha karama zetu. (4) Watu wengine katika kanisa lako (hususani viongozi) wanasema nini kuhusu karama zako? Karama za rohoni zipo ili kuliimarisha na kulitia nguvu Kanisa ili liweze kutimiza utume wake. Mwisho wa siku, kile unachofikiri kuhusu karama zako kina umuhimu mdogo sana, na badala yake cha msingi zaidi ni kile ambacho kusanyiko lako na uongozi wake wanafikiri. Hao ndio wanaojua zaidi kama Roho Mtakatifu anakutumia kwa namna fulani kuwasaidia. Ni kazi ya msingi ya wachungaji kuwasaidia watu kutambua ni karama gani za rohoni ambazo kila mshiriki anazo na kuwasaidia kukuza na kutumia karama hizo kwa njia yenye tija zaidi. Waulize viongozi wako ni karama gani wanaona ndani yako na uchukulie maanani mawazo na ushauri wao.
4
2. Roho Mtakatifu pekee ndiye anayeamua ni karama zipi kila mtu atakuwa nazo.
a. Waamini wana karama tofauti tofauti. (1) Karama hizi zinatolewa kama apendavyo Roho Mtakatifu, na zinategemea karama za wengine ili kukamilishwa na kuwa na ufanisi. (2) Warumi 12:6a
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker