Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
1 3 2 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
2. Utakatifu
a. Kanisa la Yesu Kristo ni hekalu jipya la Mungu huku kila mshirika akihesabika kuwa jiwe lililo hai (1 Pet. 2:5).
b. Baada ya kunyunyiziwa na kutakaswa kwa damu ya Kristo (Waebrania 9 na 10), sasa tunaweza kuona uwepo hai wa Roho MTAKATIFU.
c. Kama vile hekalu la Agano la Kale, Kanisa la Mungu (kwa ujumla) na kila mmoja wa washirika wake (binafsi) lazima wawe mahali pa utakatifu (Ebr. 12).
Hitimisho
» Roho Mtakatifu “Anatoa Karama” ambazo zinawawezesha watu wa Mungu kulijenga Kanisa na kutimiza kusudi lake katika ulimwengu. Karama hizi ni nguvu ya neema ya Mungu itendayo kazi kati yetu. » Roho Mtakatifu “Hukaa” ndani ya waamini ili uwepo hai wa Mungu Baba na Mungu Mwana uje katika maisha yao. Kupitia tendo la Roho kukaa ndani ya waamini, Kanisa linakuwa hekalu la Mungu aliye Hai.
4
Tafadhali pata muda wa kutosha uwezavyo kujibu maswali haya na mengine yaliyotokana na video. Unaweza ukaanza kwa kupitia kwa ufupi akrostiki ya RABBIS . Uwe wazi na mwenye kueleweka katika majibu yako, na inapowezekana, tumia Maandiko! 1. Kwanini Roho Mtakatifu anatoa vipawa kwa Kanisa? 2. Unawezaje kufafanua neno “karama za rohoni”? 3. Kuna karama ngapi za rohoni? 4. Kuna uhusiano gani kati ya karama za rohoni na vipaji vya asili?
Sehemu ya 1
Maswali ya Wanafunzi na Majibu
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker