Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

/ 1 4 7

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

* Ni kwa namna gani kusanyiko linaweza kuchukulia masuala ya dhambi na utakatifu kwa uzito na umakini mkubwa na bado likaepukana na kushikilia mno sheria na hata kuwahukumu watu? * Ni maswali gani unaweza kuuliza, na ni Maandiko gani unaweza kuyarejelea ili kumshauri Mkristo ambaye ana hofu kwamba huenda Mungu hampendi na hayuko tena pamoja naye?

MIFANO

Je, Una Karama?

Randy amekuwa Mkristo kwa takriban mwaka mmoja. Ni wazi kwamba ameendele kukua katika upendo wake kwa Mungu na kwa wengine tangu alipookoka. Randy hajui kusoma vizuri lakini amehudhuria mafunzo ya Biblia kwa uaminifu na ana hamu ya kujua Maandiko. Ingawa anapata shida kuwashirikisha wengine kwa ufasaha kuhusu mpango wa wokovu, amewaalika wafanyakazi wenzake kutoka Wal-Mart anakofanya kazi kuhudhuria ibada za kanisa pamoja naye na kadhaa miongoni mwao wamekuja. Mwezi uliopita Mchungaji Kiongozi alikuwa na mfululizo wa mahubiri kuhusu karama za rohoni. Randy ana shauku ya kulitumikia kanisa lakini anahisi kama hawezi kutambua karama za rohoni alizonazo ni zipi. Anakuja kwako kuhitaji ushauri akisema: “Sina hakika hata kama nina karama yoyote ya rohoni. Na kama ninayo, hakika sijui jinsi ninavyoweza kuigundua.” Wewe ungemwambia nini Randy? Anita amekuwa na maisha magumu. Baba yake alimnyanyasa kingono tangu alipokuwa na umri wa miaka minane hadi alipotoroka nyumbani akiwa na umri wa miaka kumi na sita. Mara tu alipokuwa mitaani aligeukia ukahaba ili kujikimu na kutumia madawa ya kulevya ili kupunguza uchungu na aibu yake. Miaka kumi iliyopita alimpa Yesu maisha yake na kuanza kuhudhuria ibada katika kanisa lako. Baada ya miezi tisa yenye utukufu, furaha na uhuru, tabia zake za zamani zilianza kujirudia. Tangu ajiunge na kanisa, Anita amekuwa katika programu ya matibabu ya uraibu wa madawa ya kulevya mara tatu, amekamatwa kwa ukahaba mara moja, na ameiba vitu kadhaa ambavyo ni mali ya kanisa na vingine ni vya waamini wa kanisa. Mara zote anaonyesha kujutia matendo yake na kurudi tena kumfuata Kristo. Hii kawaida huchukua kati ya miezi sita hadi mwaka na baada ya hapo anaangukia tena katika dhambi za zamani. Ikiwa ungetakiwa kumshauri Anita na kumsaidia kukua kama mfuasi wa Kristo, ungefanya nini? Kutengwa kwa Ajili ya Makusudi Matakatifu ya Mungu

1

4

2

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker