Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

1 6 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Roho Anayemfanya Mungu Ajulikane

Ibada

Soma 1 Wakorintho 2:10-11 na Warumi 8:26. Roho wa Mungu ni wa ajabu sana. Kwa upande mmoja, anafunua mafumbo ya ndani kabisa ya nia na mapenzi ya Baba. Ana maarifa na ufahamu usio na kikomo. Na bado, kwa upande mwingine, anayo huduma maalum ya kuwa karibu nasi, ili kutusaidia kuelewa Mungu ni nani na ni kitu gani anatamani kwetu. Roho Mtakatifu, kwa mujibu wa mafundisho ya 1 Wakorintho 2, ndiye anayetufunulia hekima na siri za Mungu zilizofichika. Na, kama vile somo la Warumi linavyoonyesha, Roho huomba mapenzi ya Mungu ndani yetu na kupitia sisi wakati ambapo fahamu zetu za kibinadamu zimefikia kikomo na hatujui nini au jinsi gani tunapaswa kuomba. Tunapoanza somo letu la theolojia ya Roho Mtakatifu, tunakumbana na kweli kuu kwamba hatuwezi kumwelewa Roho wa Mungu pasipo msaada wa Roho wa Mungu. Ikiwa kwa kweli tutaufahamu ukweli huu, utaweza kuzalisha unyenyekevu na shukrani ndani yetu. Tunanyenyekezwa kwa sababu tunatambua kwamba hatuwezi kumjua Mungu kwa juhudi zetu wenyewe (haijalishi tunajifunza kwa bidii kiasi gani), bali kwa kazi ya Roho pekee. Tunashukuru kwa sababu tunajua kwamba tumempokea Roho kupitia ahadi za kweli za Mungu na kwamba tayari yuko kazini ndani yetu na kati yetu ili kutuongoza kwenye kweli yote. Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (iliyo katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Eh! Baba mwenye neema na mtakatifu, utupe hekima ya kukufahamu, akili ya kukuelewa, bidii ya kukutafuta, subira ya kukungojea, macho ya kukutazama, moyo wa kukutafakari, na maisha ya kukutangaza kwa uweza wa Roho wa Yesu Kristo Bwana wetu. Amina. ~ St. Benedict. From William Lane, S. J. Praying with the Saints . Dublin, Ireland: Veritas, 1989. uk. 26.

1

Kanuni ya Imani ya Nikea na Sala

Hakuna jaribio katika somo hili.

Jaribio

Hakuna Maandiko ya kukariri katika somo hili.

Uhakiki wa Kukariri Maandiko

Hakuna kazi katika somo hili.

Kazi za kukusanya

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker