Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
1 8 2 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Mifano ya Matamko ya Kimadhahebu kuhusu “Ubatizo katika Roho Mtakatifu” (muendelezo)
na mapenzi makuu ya Kristo. Kujazwa na Roho kunamaanisha kutawaliwa na Roho kama inavyoonyeshwa na Paulo katika Waefeso 5:18-19. Kwa kuwa madhihirisho ya kikarismatiki [karama] yalikuwa muhimu katika kulisaidia kanisa la kwanza kufanikiwa katika kutekeleza Agizo la Kristo, kwa hiyo, sisi nasi, tunaamini kwamba kujawa na Roho Mtakatifu ni kwa lazima kwa wanadamu wote leo.
Muungano wa Makanisa ya Vineyard Imetolewa kutoka katika tamko la imani la Vineyard (The Vineyard Statement of Faith), www.vineyardusa.org/about/beliefs/beliefs_index/faith/paragraph_07.htm
Mtazamo Mchanganyiko: Wa Karismatiki
TUNAAMINI kwamba Roho Mtakatifu alimiminwa kwa Kanisa kwa nguvu siku ya Pentekoste, akiwabatiza waamini katika Mwili wa Kristo na kuachilia vipawa vya Roho kwao. Roho huleta uwepo wa kudumu wa Mungu ndani yetu kwa ajili ya ibada ya kiroho, utakaso binafsi, kujenga Kanisa, kutoa vipawa kwa ajili ya huduma, na kurudisha nyuma ufalme wa Shetani kwa kufanya uinjilisti kwa ulimwengu kwa njia ya kutangaza Neno la Yesu na kufanya kazi za Yesu. TUNAAMINI kwamba Roho Mtakatifu anakaa ndani ya kila mwamini katika Yesu Kristo na kwamba Yeye ndiye Msaidizi, Mwalimu na Kiongozi wetu wa kudumu. Tunaamini katika kujazwa au kutiwa nguvu na Roho Mtakatifu kwa ajili huduma leo. Tukio hili mara nyingi linalohusisha ufahamu. Tunaamini katika huduma ya sasa ya Roho na katika matumizi ya karama zote za Roho za kibiblia. Tunawekea watu mikono kwa ajili ya kutiwa nguvu na Roho, kwa ajili ya uponyaji, na kwa ajili ya uthibitisho na uwezeshwaji wa wale ambao Mungu amewaweka kuliongoza na kulitumikia Kanisa.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker