Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

/ 1 8 9

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Maeneo Ambayo Wakristo Wanatofautiana Kuhusiana na Karama za Rohoni (muendelezo)

b. Waefeso 2:10 – Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.

4. Kwamba hata wale ambao hawajaokoka na walio katika uasi dhidi ya Mungu wategemee uumbaji wake na karama za neema kwa ajili ya uhai wao na kuwa na tija (japokuwa zimekandamizwa, zimepotoshwa, au kuelekezwa katika njia ya uovu).

a. 1 Wakorintho 4:7 – Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea? (Linganisha na Zab. 104.)

b. Mathayo 5:45- …ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni. Maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

c. “Mungu yeye yule ndiye Mungu wa uumbaji na wa uumbaji mpya, atendeaye kazi hayo yote mawili kwa mapenzi yake makamilifu…. Kusudi lenye neema la Mungu kwa kila mmoja wetu ni la milele. Liliundwa na hata “kutolewa” kwetu katika Kristo “tangu milele iliyopita” (2 Tim. 1:9, kama lilivyo); Mungu alituchagua tuwe watakatifu na akatuweka kuwa wana wake kupitia Yesu Kristo “kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu” (Efe. 1:4,5); na kazi njema ambazo kwa ajili yake tuliumbwa upya katika Kristo ni zile hasa “ambazo Mungu alizitayarisha tangu mwanzo.” Ukweli huu wa msingi kwamba Mungu alipanga mwisho tangu mwanzo unapaswa kutuonya dhidi ya … [kutenganisha kwa urahisi sana] … kati ya asili na neema, kati ya maisha yetu kabla ya kuokoka na maisha yetu ya baada ya kuokoka” (John R. W. Stott, Baptism and Fullness: The Work of the Holy Spirit Today).

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker