Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

1 9 4 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Maeneo Ambayo Wakristo Wanatofautiana Kuhusiana na Karama za Rohoni (muendelezo)

1. Huduma ya Yesu na mfano wa Mitume na Kanisa la Agano Jipya ni kielelezo chetu kilichovuviwa kwa ajili ya huduma na wote walitumia karama za miujiza katika huduma.

2. Wakati pekee ambapo Maandiko yanazungumzia swali la lini karama zitakoma yanarejelea kurudi kwa Kristo (1 Kor. 13:8-12).

3. Roho Mtakatifu ana uhuru na ni mwenye enzi. Anaweza kutoa (au kutokutoa) karama yoyote wakati wowote kwa kusudi lolote kama apendavyo ( 1 Kor. 12:11 – anatoa atakavyo yeye).

4. Andiko la Craig S. Keener (Gift and Giver— kurasa za 89-112 ) linatoa hoja za msingi kwa mtazamo huo kwamba zote zinapatikana.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker