Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 3 9
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
c. Moto – Kinga ya Maisha (au utakaso wa Maisha). Ulimwengu wa zamani haukuwa na dawa za kuua vijidudu. Njia kuu ya kusafisha na kutakasa ilikuwa ni kutumia moto. Takataka zilichomwa ili zisiwe mahali ambapo vijidudu vya magonjwa vingezaliana (Law. 8:17). Ugonjwa ulipozuka, mara nyingi kuchoma nguo za mtu aliyeambukizwa ilikuwa njia pekee ya kuzuia ugonjwa huo usienee (Law. 13:47-59). Moto pia ulisafisha metali na kuzifanya kuwa safi na bora kwa matumizi (Mal. 3:2-3). Katika Maandiko yote Mungu anatumia ishara ya moto kuzungumzia utakaso wa watu wake. Kwa mfano, nabii Isaya anazungumza kuhusu siku “Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza” (Isa. 4:4). (1) Mathayo 3:11-12 (2) Matendo 2:3-4 (3) 1 Wathesalonike 5:19 (4) Roho Mtakatifu kama moto wa Mungu, hulitakasa Kanisa daima, akililinda dhidi ya maambukizi ambayo dhambi inaweza kuleta. d. Hua (njiwa) – Ishara ya maisha mapya Katika Mwanzo sura ya 8, wakati Mungu ameharibu uhai wote duniani kwa sababu ya dhambi, ni Nuhu tu, jamaa zake, na kundi la wanyama waliobaki hai kwenye safina. Wanapongojea maji yapungue, wanatuma njiwa ili waone kama anaweza kupata mahala penye nchi kavu. Hapo awali, kama vile Roho Mtakatifu wakati wa uumbaji, njiwa “anaruka juu ya maji” lakini hawezi kupata mahali pa kutua, na kwa sababu hiyo anarudi kwenye safina. Anatumwa mara ya pili na safari hii anarudi na jani la mzeituni linaloashiria kwamba kiwango cha maji kimepungua. Mara ya tatu anapotumwa hakurudi tena na hivyo Nuhu anajua kuwa nchi kavu imeonekana na ni salama kutoka kwenye safina na kuanza maisha tena duniani. Katika hadithi ya Nuhu, njiwa anakuwa ishara ya uumbaji mpya na matumaini mapya kwa dunia.
1
Ibid. uk. 40, 110.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker