Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

4 6 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

ya Uungu. Kama Bwana, anapewa ibada na utukufu pamoja na Baba na Mwana. Roho Mtakatifu ndiye Mpaji wa Uzima: Muumba na Mtegemezaji wa maisha yote. Amepewa alama na vyeo katika Maandiko ambavyo hutusaidia kuelewa zaidi kazi yake ya kutoa uzima. Yeye pia ndiye anayetoa uzima mpya (hufanya upya); kwanza kwa njia ya kuzaliwa upya ambapo watu wanafanyika viumbe vipya katika Kristo; na siku moja katika wakati ujao ataizaa mbingu mpya na nchi mpya, makao ya haki. Ikiwa utapenda kupata ufahamu wa kina zaidi kuhusu baadhi ya maarifa yaliyomo katika somo hili la Nafsi ya Roho Mtakatifu, basi unaweza kuangalia vitabu hivi: Bickersteth, EdwardHenry. The Trinity . GrandRapids, MI: Kregel Publications, 1977. Saint Basil. On the Holy Spirit. Crestwood, NY: St. Vladimir’s Seminary Press, 1980. Pia vinapatikana kama vitabu vya kusomea mtandaoni katika tovuti zifuatazo: • www.newadvent.org/fathers/3201000.html • www.monachos.net/patristics/basil/on_holy_spirit_a.shtml Sasa ni wakati wa kujaribu kukazia theolojia hii kwa kuitumia katika huduma halisi. Ni kweli gani kutoka katika somo hili ambazo Mungu amezifunua na kuziangazia kipekee katika moyo wako? Ni hali gani hasa inakuja akilini unapofikiria kuhusu kuwafundisha watu kuelewa fundisho la Roho Mtakatifu? Ni sehemu gani ya somo hili utatumia muda kuitafakari na kuiombea kuelekea juma lijalo. Kutafakari juu ya Nafsi ya Roho Mtakatifu kumekuwa changamoto na kazi ngumu katika historia ya Kanisa. Umeitwa kuingia katika mkondo huu mrefu wa tafakuri ya kitheolojia na kuona matokeo ya kivitendo kwa wale unaowaongoza na kuwafundisha. Kwa bahati nzuri, unaweza kumwomba Roho Mtakatifu mwenyewe aweze kukusaidia kuelewa kweli hizi zenye kina na kukupa mwongozo wa moja kwa moja juu ya namna ambavyo kweli hizi zinapaswa kuathiri maisha na huduma yako. Usiache kumwomba Roho akupe mwanga zaidi juu ya Maandiko ambayo tumejifunza. Ataweka wazi maana na manufaa ya Maandiko hayo. Sala ambayo iko katika sehemu inayofuata inakupa mwanzo mzuri juu ya hili.

Nyenzo na Bibliografia

1

Kuhusianisha somo na huduma

Roho Mtakatifu wa Mungu, “Unifumbue macho yangu niyaone mambo ya ajabu yaliyomo katika Neno lako.” Ufahamu wangu una mipaka, ufahamu wako hauna kikomo. “Naona kupitia kioo katika giza,” Wewe unachunguza mawazo

Ushauri na Maombi

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker