Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
5 6 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
I. Unabii ni Nini ?
Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video
A. Ufafanuzi: unabii ni njia ya kuijua kweli ambayo inakuja kwa njia ya ufunuo wa moja kwa moja kutoka kwa Mungu.
1. Neno la Kiyunani proph ē t ē s (nabii):
a. Pro (likiwa na maana “kabla” au “kwa niaba ya…”)
b. Ph ē mi (likiwa na maana “kuongea”)
2
c. Nabii ni mtu anayezungumza kwa niaba ya mtu fulani au mbele ya mtu fulani (yaani mtu anayetangaza ujumbe). Kwa hiyo, ufafanuzi wa kimapokeo wa nabii kibiblia ni “anenaye kwa niaba ya Mungu mbele ya watu.”
Kuna maneno matatu ya Kiebrania yanayotumika katika tafsiri za neno “nabii”: nãbî , r ’eh na h zeh . Hili la kwanza mara zote linatafsiriwa kama “nabii”, wakati ambapo la pili, ambalo lipo katika tatu, pia ni kanuni ya kitenzi kingine yenye maana ya “kuona”, na kwa bahati mbaya halina neno mahususi katika Kiingereza na hivyo hutafsiriwa ama kama “nabii” (m.f. Isa. 30:10) au kama “mwonaji” (m.f. 1 Nya. 29:29). ~ “Prophecy.” New Bible Dictionary , 2nd ed. uk. 976. kitenzi kitendaji kishiriki “kuona” linatafsiriwa kama “mwonaji”, na la
2. Unabii ni ujumbe unaokuja moja kwa moja kutoka kwa Mungu.
a. Yereremia 1:9
b. Mwanatheolojia W. E. Vine anasema kwamba nabii ni: “yeye anayesema waziwazi. . . mtangazaji wa ujumbe wa kimungu. . . . yeye ambaye Roho wa Mungu anakaa juu yake... yeye ambaye kwake na kupitia kwake Mungu hunena” ( Vines Complete Expository Dictionary of Old and New Testament Words, uk. 493).
3. Maandiko yote ni ya kinabii, yaani ni ufunuo wa kweli uliotoka moja kwa moja kwa Mungu kupitia waandishi waliovuviwa.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker