Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

5 8 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

b. Maandiko yanayojulikana kama “Manabii” ni yale ambayo kwa sehemu kubwa yamejumuisha maneno yaliyotolewa na manabii wanaotambulika. Unabii huu hasa ulilenga kuwaita Waisraeli wasiotii warudi katika ibada ya kweli na hali ya kujitoa kwa uaminifu kwa Yahwe. c. Mwandishi wa Torati au Sheria ndiye Nabii Mkuu wa Israeli. (1) Musa aliandika vitabu vya Sheria (Torati), na si vitabu vya kinabii. (2) Musa ni Nabii Mkuu wa Agano la Kale. Anasimama kama kipimo cha huduma zote za kinabii zilizofuata baada yake, na yeye mwenyewe ndiye kielelezo cha huduma ya kinabii ya Masihi. (3) Kumbukumbu 34:10 (4) Kumbukumbu 18:15 (taz. Matendo ya Mitume 3:22; 7:37). d. Yeyote anayeandika chini ya uvuvio wa Roho wa Mungu anaandika kinabii hata kama kile anachoandika kinaweza kisiwekwe katika fungu la Maandiko inayojulikana kama “vitabu vya kinabii.” Kwa mara nyingine, katika maana pana zaidi, Maandiko yote ni unabii, si sehemu fulani tu ndani yake, kwa sababu Maandiko yote ni kweli iliyoletwa kwetu kupitia ufunuo wa moja kwa moja kutoka kwa Mungu.

2

Matumizi mapana ya neno [nabii] yanaeleza kwa nini Baba wa Imani Ibrahimu (Mwa 20:7), Kuhani Haruni (Kut. 7:1), na Mwimbaji Yeduthuni (1 Nya. 25:3) wote waliitwa Manabii ingawa Maandiko hayana kumbukumbu ya wito wao katika Ofisi ya Kinabii. ~ International Standard Bible Encyclopedia , Toleo la 3. uk. 986.

3. Dhana potofu ya #3: Manabii wote ni Wanaume.

a. Maandiko yanazungumza kuhusu Manabii wa Kike wengi (1) Miriamu, Dada yake Musa, Kut. 15:20

(2) Debora, Waamuzi 4:4 (3) Hulda, 2 Nya. 34:22 (4) Anna, Luka 2:36

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker