Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 6 1
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
1. 1 Wakorintho 12:4-11
2. Warumi 12
3. 1 Wathesalonike 5:19-21
C. Maandiko ya Agano la Kale na Agano Jipya yamevuviwa na Roho Mtakatifu.
1. Fundisho la Uvuvio (Inspiration) .
2
a. Ufafanuzi: Neno Uvuvio wa Maandiko linamaanisha ule ushawishi wa kiungu wa Roho Mtakatifu juu ya waandishi wa Maandiko ambao ulipelekea maandishi yao yawe kumbukumbu sahihi ya ufunuo, au ambao ulisababisha kile walichoandika kuwa Neno la Mungu (Millard Erickson, Introducing Christian Doctrine, uk. 61). b. Maandiko yenyewe yanashuhudia kwamba yameandikwa na Roho Mtakatifu. (1) Roho alinena kupitia Daudi, 2 Sam. 23:1-2. (2) Manabii wa Agano la Kale waliongozwa na Roho Mtakatifu na sio matakwa yao wenyewe, 2 Pet. 1:20-21. (3) Yesu alithibitisha kwamba Daudi alinena kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu, Mt. 22:43. (4) Wakristo wa kwanza walithibitisha kwamba Daudi alinena kwa njia ya Roho Mtakatifu, Matendo ya Mitume 4:25. (5) Paulo anasema kwamba Maandiko yote yana “pumzi ya Mungu”, 2 Tim. 3:16. (6) Maandiko ya Agano la Kale yananukuliwa kama sauti halisi ya Roho Mtakatifu, Ebr. 3:7.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker