Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

6 4 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

leo anapotuelekeza katika maana ya Maandiko aliyoyavuvia na kutuongoza kutii mafundisho ya Kristo kwa uaminifu. Jibu maswali haya kwa uwazi na ufasaha, na inapowezekana, jenga hoja kwa kutumia Maandiko! 1. Toa tafsiri pana ya “unabii”, kisha eleza tafsiri nzuri ya “nabii”. 2. Ni dhana gani potofu ambazo mara nyingi watu wanazo kuhusiana na unabii? Ni matatizo gani dhana hizi potofu zinaweza kusababisha? 3. Unabii unaweza kuhusisha kutabiri (kuwasilisha ujumbe wa Mungu) kwa ajili ya wakati wa sasa (forthtelling), wakati kwa sehemu unabii unahusisha pia kutabiri matukio ya wakati ujao (foretelling). Nini tofauti kati ya dhana hizo? Maana hizi mbili za unabii zinahusianaje ?

4. Kiasi gani cha Maandiko ni unabii? Unajuaje? 5. Elezea kazi ya Roho Mtakatifu katika unabii.

2

6. Nini maana ya kitheolojia ya neno uvuvio? Inatofautiana vipi na namna tunavyoweza kutumia neno hili [katika maana ya msukumo, ushawishi, kuvutia au kutia hamasa] katika mazungumzo ya kila siku? 7. Nini maana ya kitheolojia ya neno kuangazia (kutia nuru)? Kuna uhusiano gani kati ya kuangaziwa na uvuvio?

Kazi ya Kinabii ya Roho Mtakatifu Sehemu ya 2: Roho Anayetuhakikisha kwa Habari ya Dhambi Zetu

Mch. Terry G. Cornett

Katika sehemu hii ya pili, tutatilia mkazo ukweli kwamba Roho wa kinabii ndiye anayetuhakikisha kwa habari ya dhambi zetu. Kila wakati Roho anapozungumza kiunabii, anatafuta kutuvuta kuyaelekea mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo, kazi ya unabii ya Roho Mtakatifu haijumuishi tu ufunuo wa mapenzi ya Mungu bali pia huduma inayoendelea ambayo kwayo Roho hutushuhudia kwa habari ya hali yetu ya kutomtii Mungu na hutuwezesha kwa neema kutubu dhambi zetu na kumgeukia Mungu. Kazi hii ya kutuhakikisha aifanyayo Roho Mtakatifu ndiyo mada ya sehemu hii.

Muhtasari wa Sehemu ya 2

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker