Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
6 6 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
a. Zabarui 53:2-3 - Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu. 3 Kila mtu amepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.
Martin Luther alikuwa sahihi aliposema, “wenye kiburi hawaijui ladha ya neema kwasababu dhambi zao bado hazijawa chungu kwao” ( Luther’s Works , Jaroslav Pelikan, ed. St. Louis: Concordia, 1958, 14:166).
b. Yeremia 17:9 – Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?
2. Yesu alimtuma Roho Mtakatifu waziwazi kuuhakikisha ulimwengu kuhusu dhambi, Yohana 16:7-8.
2
3. Hotuba ya kinabii hutoka kwa Roho Mtakatifu na kumtia hatiani asiyeamini kwa habari ya dhambi kwa kuufunua moyo wake (1 Kor. 14:24-25; Ebr. 4:12).
4. Mahubiri na mafundisho ya Neno la Kinabii linalopatikana katika Maandiko ni njia ya msingi ambayo Roho Mtakatifu huitumia kuuhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi.
a. Matendo ya Mitume 2:37 (ling. Rum. 10:14-17)
b. Matendo ya mitume 8:26-38.
c. Tazama pia: Mt. 4:17; Rum. 3:20; 1 Kor. 1:21; 2 Tim. 4:2.
II. Kazi ya Roho Mtakatifu katika Toba
A. Maneno mawili ya msingi ya kibiblia yanayomaanisha toba.
1. Agano la Kale
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker