Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

6 8 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

b. “Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani,” Rum. 8:6.

c. Tumeitwa kwenye kufanywa upya nia zetu, Rum. 12:2 (ling. Efe. 4:17-18).

d. Kuungama dhami ndiyo ishara inayoonekana zaidi kuhusu badiliko la nia. Tunatambua na kuwa radhi kuviita dhambi vitu ambavyo mwanzo tulivihalalisha au kuvipuuza (Mit. 28:13; 1 Yoh. 1:8-9).

2

2. Toba inajumuisha badiliko la MOYO .

a. Neno la kibiblia la badilko hili la moyo ni “majuto” au kujutia. (1) Kujutia ni kuwa na huzuni inayoambatana na unyenyekevu kwa sababu ya dhambi. (2) Neno la kiebrania “kujuta” [ dâkâ ] kimsingi linamaanisha “kuvunjika vipandevipande” au “kupondeka.” (3) Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliyovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau, Zab. 51:17. b. Majuto ya kweli: (1) “Kutetemeka”usikiapo Neno la Bwana, Isa. 66:2. (2) Huonyesha ishara za kimwili na kimatamshi za unyenyekevu, Luka 18:13. (3) Inaitwa “huzuni ya kimungu,” 2 Kor. 7:10. (4) Huonyesha hisia za kweli za huzuni dhidi ya dhambi, Yoeli 2:12; Zek. 12:10-13:1, na msiba, Yoeli 2:12. (5) Tumekwisha taja neno la Kiebrania linalomaanisha toba, shubh, ambalo lina maana ya “kugeuka.” Kuna neno la kiebrania la pili kuhusu toba, nâcham, ambalo pia linatumika katika maeno

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker