Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 8 3
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Kumfahamu mtu fulani maana yake nini hasa?
Ikiwa mtu angesema kwamba anakujua vizuri, angekuelezeaje? (Tengeneza orodha fupi ya baadhi ya mambo anayoweza kusema). Unapotazama orodha yako, ni mambo mangapi kati ya hayo yanakuelezea wewe ni nani (kwa mfano, mchangamfu, mvumilivu, rafiki, Mwasia, mwanamume, n.k.) na ni mangapi kati ya hayo yanayoelezea kile unachofanya (kwa mfano, kurekebisha magari, mchezaji wa mpira wa kikapu, anafanya kazi Wal-Mart, anatazama filamu nyingi)? Je, aina hizi mbili tofauti za maelezo zinatoaje mwanga kuhusu wewe ni nani hasa? Katika theolojia, tunamwelezea Mungu kwa njia mbili: nafsi yake (yeye ni nani, ikimaanisha tabia yake, asili yake, na sifa zake) na kazi yake (kile anachofanya). Tunapozungumza kuhusu nafsi na kazi yaMunguRohoMtakatifu, kilamoja ya haya hutuambia jambo muhimu kumhusu Yeye. Katika masomo mawili yanayofuata, tutajikita zaidi katika ufahamu juu ya kazi ya Roho Mtakatifu. Kujua anachofanya kunaweza kutuambia jambo muhimu kuhusu Yeye ni nani. Tunapojiandaa kuanza somo hili, tengeneza orodha ya haraka inayoelezea kazi nyingi za Roho Mtakatifu kadri unavyoweza kufikiria kwa dakika moja. RohowaMungu ndiye anayewavuta waamini wote kilamahali katika umoja. Mtume Paulo, kwa hakika, anatuambia “tudumishe umoja wa Roho katika kifungo cha amani” (Efe. 4:3). Hata hivyo likitajwa suala la “ubatizo katika Roho Mtakatifu”, Wakristo mara nyingi sana huanza kugombana wao kwa wao juu ya maana yake, ni wakati gani jambo hilo hutokea, na nini kinaonyesha kwamba limetokea kwa mtu. Kwa kuzingatia mapokeo yako mwenyewe, uzoefu, na usomaji wa Maandiko, ungejibuje swali, ‘‘Ubatizo katika Roho Mtakatifu ni nini?” na “Je, imekuwa rahisi kufanya kazi pamoja na akina kaka na akina dada Wakristo ambao wanauelewa kwa namna tofauti na unavyouelewa? Ikiwa ndiyo, eleza namna gani; ikiwa hapana eleza kwa nini.” Ubatizo katika Roho Mtakatifu
2
3
3
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker