Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 9 5
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Uwepo wenye Nguvu wa Roho Mtakatifu (Sehemu ya Kwanza) Sehemu ya 2: Ubatizo katika Roho Mtakatifu
Mch. Terry G. Cornett
Katika sehemuyakwanza tulilengakuonyeshakwambaRohondiye anayetuwezesha kuzaliwa mara ya pili (kiroho) na kutuingiza katika familia ya Mungu, kwa kutuzaa upya na kutuasili, yaani kutufanya kuwa wana. Katika sehemu hii ya pili, tutazungumza kuhusu taswira ya kibiblia ya “kubatizwa katika Roho wa Mungu” na jukumu ambalo Roho huchukua katika kuwaunganisha waamini na Kristo na kuwawezesha kuhudumu katika Jina lake. Lengo letu la sehemu hii, Ubatizo katika Roho Mtakatifu, ni : • Kuwakumbusha wanafunzi kwamba ubatizo wa Roho Mtakatifu ni fundisho muhimu la kibiblia. • Kueleza baadhi ya vipengele muhimu vya kazi ya Roho katika kutuunganisha na Kristo. • Kuwasaidia wanafunzi kuelewa kwamba kuna maeneo ambayo wakristo hawakubaliani kuhusiana na ubatizo wa Roho ikiwa ni pamoja na kile ambacho ubatizo huo unatimiza, na wakati na jinsi gani unafanyika. • Kuwawezesha wanafunzi kufanya muhtasari wa mitazamo inayotawala kuhusiana na ubatizo wa Roho na kuona jinsi kila mmoja wa mitazamo hiyo unavyotetewa kwa kutumia Maandiko. • Kuwasaidia wanafunzi kuelewa na kutetea msimamo wao wenyewe juu ya ubatizo wa Roho na pia kuelewa na kujifunza kutoka katika mitazamo ya wengine.
Muhtasari wa Sehemu ya 2
3
Tutaendelea kutumia akrostiki ya RABBIS ili kuelewa huduma ya Roho Mtakatifu tunapojadili “B” ya kwanza - ubatizo ( b aptism ) katika Roho Mtakatifu.
I. Utangulizi
Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video
A. Hii ni mada ya kitheolojia ambayo ina mitazamo na imani tofauti kabisa ndani ya Kanisa la Kristo! Hakuna njia ya kutatua kabisa kutokubaliana
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker