Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
9 8 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
a. Kipawa cha Roho Mtakatifu kilisababisha Kanisa kuzaliwa, Matendo 2:38-39.
b. Kipawa cha Roho Mtakatifu kinatuunganisha na Kristo na Kanisa lake (1 Kor. 12:13; Efe. 4:4-6).
Kwa mujibu wa Paulo kipawa cha Roho ni mwanzo wa maisha ya Kikristo (Gal. 3:2 3), njia nyingine ya kuelezea uhusiano mpya wa kuhesabiwa haki (1 Kor. 6:11; Gal. 3:14; Tito 3:7). Vinginevyo, mtu hawezi kuwa wa Kristo isipokuwa awe na Roho wa Kristo ( Rum. 8:9 ), mtu hawezi kuunganishwa na Kristo isipokuwa kwa njia ya Roho ( 1 Kor. 6:17 ), mtu hawezi kushiriki uwana wa Kristo bila kuwa na Roho wake ( Rum. 8:14-17; Gal. 4:6-7), mtu hawezi kuwa kiungo cha Mwili wa Kristo isipokuwa kwa kubatizwa katika Roho (1 Kor. 12:13). ~ J. D. G. Dunn. New Bible Dictionary . uk. 1139. c. Utetezi wa kimaandiko wa kanuni kuu za kitheolojia (1) Kupitia ubatizo katika Roho, tunaunganishwa na Kristo. (a) Warumi 8:9 (b) Yohana 7:37-39 (c) 1 Wakorintho 6:17 (d) Hakuna anayeweza kudai kuwa anamjua Kristo ikiwa hajapitia tendo hili hai la kuunganishwa pamoja naye kupitia umwagizo wa Roho Mtakatifu. Matokeo ya ubatizo huu katika Roho ni kwamba sasa tunaitwa tulio “ndani ya Kristo” (taz. Rum. 8:1; 16:7; 2 Kor. 5:17; Efe. 2:6-7; Kol. 2:9-10; 1 Pet. 5:14). . (e) Kwa njia ya Roho Mtakatifu, tunaunganishwa na Yesu ili
3
maisha yake yawe maisha yetu, kifo chake kiwe kifo chetu, ufufuo wake uwe ufufuo wetu, na ukaribu wake na Mungu Baba ufanyike ukaribu wetu na Yeye.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker