The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

1 0 2 /

UFALME WA MUNGU

e. Petro anarudia hitaji la kuwa na kiasi na kukesha kwani mwisho wa mambo yote umekaribia, 1 Pet. 4:7.

f. Nguvu ya neno la unabii kuathiri ufuasi wa mtu, 2 Pet. 1:19.

g. Tujitunze katika upendo wa Mungu tukitafuta rehema ya Yesu hata uzima wa milele, Yuda 1:20-21.

C. Umuhimu wa eskatolojia : Ufalme wa Mungu utatimizwa hivi karibuni, na tunapaswa kusimama tayari na kuwa macho kwa ajili ya kutokea kwake kwa mwisho na kwa utukufu.

II. Kuna uhusiano gani kati ya suala la kifo na kukamilishwa kwa utawala wa Ufalme wa Mungu?

A. Zingatia tofauti kati ya eskatolojia ya mtu binafsi na ya ulimwengu.

4

1. Eskatolojia ya mtu binafsi – mambo yajayo ya mustakabali wa watu binafsi

2. Eskatolojia ya ulimwengu – mambo yajayo ya mustakabali wa wanadamu na viumbe vyote.

B. Je, kuna kanuni gani muhimu za kibiblia kuhusu kifo katika Maandiko?

1. Kifo ni halisi kwa kila mtu na hakiepukiki.

a. Kifo ni hakika kwa kila mwanadamu.

Made with FlippingBook - Online catalogs