The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

1 0 6 /

UFALME WA MUNGU

III. Je! ni nini asili ya “Hali ya wafu,” na inahusianaje na uelewa wetu wa utimilifu wa ufalme?

A. Neno “hali ya wafu” linamaanisha nini?

1. Hali ya wafu – hali ya wanadamu kati ya kifo chao cha kimwili na ufufuo.

2. Uelewa huu ni muhimu kwa sababu inatuwezesha kuwahudumia kwa ufanisi zaidi wale ambao wamepoteza familia na marafiki mjini.

3. Ni mada gumu kusuluhisha: maandiko ni machache na mjadala ni mkali.

B. Hali ya wafu kama “usingizi wa nafsi.”

4

1. Kulala kwa nafsi ni mtazamo kwamba nafsi imelala katika kipindi cha kati ya kifo na ufufuo, katika hali ya utulivu na kupoteza fahamu.

2. Je, kuna ushahidi gani wa kibiblia kwa mtazamo huu?

a. Kuuawa kwa Stefano kunaelezewa kama usingizi, Mdo 7:60.

b. Paulo anamrejelea Daudi kama aliyelala (au kufa) baada ya kumtumikia Mungu katika kizazi chake (Mdo. 13:36).

c. Picha ya usingizi imetumika mara nne katika 1 Wakorintho 15, mst. 6, 18, 20, 51.

Made with FlippingBook - Online catalogs