The Kingdom of God, Swahili Student Workbook
1 3 2 /
UFALME WA MUNGU
* Tufanye nini kwa mamilioni yote wasiomjua Mungu katika Kristo? Je, hali yao ni ipi mara wanapokufa – ni hali gani ya kifo wanayopitia, na matokeo yao ya mwisho yatakuwa nini? * Je, kunaweza kuwa na msisitizo juu ya mambo ya eskatolojia, yaani, kuzingatia nyakati za mwisho, ambao hauzalishi aina ya kiasi na kukesha inayozungumzwa katika Biblia? Je, ni wakati gani majadiliano ya mambo haya yanakuwa tatizo, au hata kupoteza muda? * Je, ni lazima uamini katika kuzimu ya milele ili kuwa sahihi katika Imani ya Kristo ya kihistoria? * Je, masuala kama milenia na dhiki ni muhimu kwa viongozi wa Kikristo wa mijini kujua na kuweza kutetea? Kuna mipaka ya kuzingatiwa kuhusu kile ambacho ni muhimu sana katika mada hizi? Kanisa kubwa la jijini, lenye mchanganyiko wa watu wa asili na jamii mbali mbali limekuwa mahali maarufu sana kwa vijana waishio katika jij`i hilo, wanaotoka katika jamii za walio wachache, na ambao kiroho wanahitaji kuchukuliwa kwa umakini kutokana na desturi na mila za jamii wanazotoka. Kila Jumapili, mamia ya wamarekani weusi, na wale wa asili za Asia Kusini, Mashariki ya Kati, Amerika ya Latini, n.k waishio mijini huja kuabudu katika kanisa hilo linalokua kwa kasi. Pamoja na kujiuzulu kwa mchungaji wao kiongozi, kanisa hilo limeteua kamati ya kumtafuta mchungaji mpya kuchukua nafasi ya kiongozi wao mwema aliyeitwa na Mungu mahali pengine. Katika usaili wa wagombea wa nafasi ya uchungaji, kamati hiyo inaamini imepata kiongozi kwa ajili ya awamu yake ijayo. Mtu mcha Mungu aliyejaa maombi na Neno, ndugu huyu mpendwa analipenda kanisa na yuko tayari kuja, ikiwa kanisa litapenda kumwita. “Kikwazo” pekee ambacho kamati inakiona ni kwamba mtahiniwa huyu wa nafasi ya uchungaji anapenda kufundisha na kuhubiri kuhusu unabii wa Biblia, hasa juu ya matarajio ya uzima wa milele kwa waliookolewa, na laana ya milele kwa waliopotea. Kanisa ni «sikivu kwa watafutaji» katika mwelekeo wake, yaani, linatafuta kwanza kujenga madaraja ya uhusiano kupitia upendo, huduma, na urafiki kabla ya kuwaingiza watu kwenye «mambo mangumu» ya Injili. Hata hivyo,mchungaji huyu mtahiniwa amekuwa wazi kwamba anataka kuwa na uhuru wa kuzungumza juu ya hukumu ya mwisho, ufufuo, na tumaini la mbinguni. Wengine wana wasiwasi kwamba atawatisha na kuwaogopesha watu wengi, na hivyo kuwapelekea kuondoka kanisani na kupoteza fursa ya kumwamini Yesu na kujitoa kikamilifu kwa Mungu. Je, ungeishaurije kamati hii ya usaili kwa ajili ya nafasi ya mchungaji? Kuweka Mipaka katika Maeneo Sahihi
MIFANO
1
4
Made with FlippingBook - Online catalogs