The Kingdom of God, Swahili Student Workbook
/ 1 3 5
UFALME WA MUNGU
Mtihani wa mwisho utakuwa wa kwenda nao nyumbani, na utajumuisha maswali yaliyochukuliwa kutoka katika majaribio matatu ya kwanza, maswali mapya kutokana na maarifa yaliyofundishwa katika somo hili, na maswali ya insha ambayo yatahitaji majibu yako mafupi kwa maswali muhimu yenye lengo la kuhusianisha somo na huduma na maisha. Pia, wakati wa mtihani unapaswa kujiandaa kuandika au kutamka aya zilizokaririwa katika kozi hii. Ukimaliza mtihani wako, tafadhali mjulishe mkufunzi wako na uhakikishe kuwa anapata nakala yako. Tafadhali zingatia: Ufaulu wako katika moduli hii hauwezi kupimwa na kujulikana kama hautafanya mtihani wa mwisho na kukusanya kazi zote na kuzikabidhi kwa mkufunzi wako (Fomu ya Ripoti ya Usomaji, kazi za kihuduma, kazi za ufafanuzi wa Maandiko, na mtihani wa mwisho). Mungu asifiwe, umekamilisha moduli ya Ufalme wa Mungu ya Mataala wa Capstone . Hata hivyo, huu ni mwanzo tu wa safari yako ya kuchunguza na kujifunza kupitia nyenzo nyingi za maarifa ya Biblia kuhusu Ufalme wa Mungu. Mungu akupe neema na hekima ya kuutafuta kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake ili kila unachohitaji katika maisha na huduma upate kuzidishiwa. Amina.
Taarifa Kuhusu Mtihani wa Mwisho
Neno la Mwisho kuhusu Moduli Hii
4
Made with FlippingBook - Online catalogs